Na.Khadija Seif Michuzi Tv
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewakumbusha wasanii kuwa hawana lengo la kufungia kazi ya msanii bali wapo Kwa ajili ya kuzungumza na kurekebisha kazi ili kuikuza tasnia ya Sanaa kwa mapana.
Akizungumza kauli hiyo Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana wakati wa kuwapa
nasaha na baraka pamoja na kupokea maoni yao Huku akiwakabidhi bendera
washiriki wa tuzo za zikomo zilizowajumuisha wasani wa Filamu, wabunifu wa
Mavazi,wasanii wa vichekesho, watangazaji,wapiga Muziki ambao wanatajiwa kwenda
nchini Zambia kwa ajili ya kilele cha fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika
rasmi mwezi octoba Jijini Lusaka nchini Zambia.
Mapana amefafanua zaidi kuwa kwa
sasa watanzania wawapigie kura nyingi washiriki hao ambao kwa upande wa
Tanzania tunagombea tuzo 50 katika vipengele tofauti tofauti.
"Watakaoshiriki wote
tutawapatia vyeti vya kutambulika mchango wao katika ushiriki wao na kwa
washindi pia watapewa zawadi hivyo tutawaandalia usiku wao wa kuwapongeza Ili
waweze kuona basata sio sehemu ya kuwafungia tu kazi zao au kutoa vibali bali
pia no sehemu ya kuchagiza na kutoa hamasa pale taifa linapokua nje kwenye
vinyang'anyiro vya tuzo za Kimataifa."
Hata hivyo mapana amesisitiza
zaidi kuwa wasanii wanatakiwa kujisajiri basata Ili waweze kupata fursa na
vipaumbele mbalimbali vinavyotokea ikiwemo kupatiwa mikopo kwa wasani ambao
kigezo cha kwanza ni kutambulika kisheria na baraza la sanaa(BASATA).
Kwa upande wake Mbunifu wa Mavazi
nchini Martin Kadinda amewaomba basata kuwashika mkono katika safari ya
kuelekea zambia Kwa upande wa usafiri ili washiriki waweze kumudu kusafiri ili
kupata hamasa zaidi na kurudi na ushindi wao.
"Tungependa tuweze kushirikiana na shirika la ndege kuona kwa kiasi gani tunaweza kupunguziwa gharama za usafiri ili Kwa uchache wetu tuweze kufika mji wa Lusaka nchini Zambia kwenye fainali za tuzo za zikomo."
0 Comments