SUAMEDIA

Kigogo aliyefukuzwa TRC apewa dhamana

Dar es Salaam. Hatimaye aliyekuwa meneja Shirika la Reli Tanzania (TRC) kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi ameachiwa kwa dhamana, Mwananchi linazo taarifa.



 Afumwisye ameachiwa leo Agosti 31, 2022 ikiwa ni siku ya sita tangu ashikiliwe na jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, kutokana na tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kupinga tozo za miamala kwenye mitandao ya kijamii.

 Msimamo wa kupinga tozo hizo kulimsababishia, Agosti 19, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amwandikia barua Afumwisye kumjulisha kuhusu uamuzi wa kumfuta kazi baada ya kuthibitika kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili kabla ya Agosti 24 kukamatwa na Polisi.

Taarifa za kuachiwa kwake zimethibitishwa na wakili wake Peter Kibata huku akieleza kwamba pamoja na kuachiwa kwake wamewasilisha rufaa ya kupinga kufutwa kazi kwa Afumwisye.

 “Tumekata rufaa ya kupinga kufukuzwa kazi na TRC huko tume ya utumishi wa umma tangu Agosti 29 mwaka huu na imepokelewa sasa tunasubiri maelekezo ya tume namna rufaa itakavyoshughulikiwa,” amesema Kibatala


Post a Comment

0 Comments