SUAMEDIA

Wananchi waaswa kutumia Mbogamboga ili kupata virutubisho, kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa

 

Na Amina Hezron,

Morogoro

Wananchi wameshauriwa kutumia mbogamboga katika kiwango sahihi ili kuweza kupata virutubisho ambavyo vitawasaidia kuimarisha kinga mwilini na dhidi  ya magonjwa ya kuambukiza na yale yasioyambukiza.

Mtaalamu wa Lishe kutoka katika Idara ya Lishe na Sayansi ya Mlaji Prof Joyce Kinabo akizungumza katika kipindi cha kapu la leo kuhusu umuhimu wa Mbogamboga 


Akizungumza kwenye kipindi cha Kapu la Leo kinachorushwa na SUA FM, Prof. Joyce Kinabo ambaye ni mtaalamu wa lishe kutoka Idara ya Lishe na Sayansi ya Mlaji Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) amesema kuwa ulaji wa mboga za majini unasaidi upatikanaji wa potasiamu ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ugonjwa wa  shinikizo la kiwango cha juu la damu.

“Wale ambao hawali mboga za majani wanaathirika zaidi na magonjwa mengi na hasa kwa wale ambao wanazoea kula nyama zaidi ‘antioxidants’ zilizopo kwenye mboga mboga zinasaidia kupunguza msukosuko unaotokana na ulaji wa kiasi kingi cha nyama ama vyakula vyovyote vya protini ambayo vinaweza kuathiri mwili wa binadamu”, amesema Prof.  Kinabo.

Prof.  Kinabo ameeleza kuwa mboga mboga iandaliwe wakati ambao itakuwa tayari kwa kuliwa hivyo inapochumwa inatakiwa kutumika mara moja ioshwe vile ilivyo ikatwe ipikwe wakati huohuo na kuliwa ili kuepeka kupoteza virutubisho kwenye maji  hali za hewa na mwanga.

“ Mboga mboga inatakiwa kupikwa kwa mudo usiozidi dakika 15 ukipika kwa muda mrefu virutubisho vingi vinapotea ambapo katika uandaaji  wa chakula mboga ipikwe wakati ambao tayari vyakula vingine vimeshakuwa tayari ili utakapotoa jikoni iweze kuliwa muda huo huo ”, Prof.  Profesa Kinabo.

Prof.  Kinabo amefafanua kuwa uandaaji wa mboga kwa ulaji wa baadaye ama kesho yake hauna faida katika kuleta virutubisho mwilini kwa kuwa vijidudu viharibifu vitakuwa vimeshazaliwa na kuharibu mboga mboga .

Aidha amewataka wazalishaji wasizalishe mboga mboga kwa kuzingatia pesa tu bali wazalishe kwa kuzingati lishe na afya za walaji ili kuwaepesha na magonjwa yatokanayo na ulaji wa mboga mboga ambazo si salama.

 

Post a Comment

0 Comments