Winfrida Nicolaus
Imeelezwa kuwa unyweshaji wa maziwa kwa ndama sharti ufanywe
katika hali ya usafi ili kuondoa uwezekano wa ndama kuharisha au kupata
magonjwa ikiwemo Nimonia vilevile muda wa kumlisha au kumnywesha ndama
unatakiwa uwe sawa kila siku na joto la maziwa lisibadilike.
Hayo yamesemwa na Msimamizi wa shamba la malisho katika shamba
la mfano katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Jontus Karoli
wakati akizungumza na SUAMEDIA
Bw. Karoli amesema baadhi magonjwa kwa ndama hutokea hasa
wakati wa unyweshaji wa maziwa hivyo mfugaji anatakiwa kuhakikisha kuwa vifaa
anavyotumia katika unyweshaji maziwa vinakuwa safi na salama ikiwemo mikono,
kucha za wastani pamoja na kuwa nafya njema yaani kutokuwa na magonjwa hasa
yale ya kuambukiza kama TB, magonjwa ya kuharisha na mafua kwa kuwa kuna
magonjwa ambayo hutoka kwa binadamu kwenda kwa mifugo na kutoka kwa mifugo
kwenda kwa binadamu.
Amesema usafi pekee kati zoezi la unyweshaji maziwa kwa ndama
ndio unaolinda afya yake lakini pia mfugaji anatakiwa kuhakikisha anatunza muda
na joto la maziwa kwakuwa maziwa yakipoteza joto lake yanaenda kusimama tumboni
na kuleta shida katika umeng`enywaji wa chakula kwa ndama na baadae
kumsababishia kuhara.
‘‘Kwa wale wanaotumia ndoo katika unyweshaji wa maziwa kwa
ndama ndoo ya chuma ‘aluminium’ ni nzuli zaidi na si ya plastiki kwa kuwa ya
plastiki inatabia ya kutunza uchafu, mafuta pamoja na halufu na unapomalizia tu
kunywesha osha vifaa kwa maji ya kutosha ikiwezekana tumia maji ya moto’’
Amesema Jontusi Karoli
Bw. Karoli ameongeza kuwa tofauti na kuhara kuna baadhi ya
magonjwa mengine ambayo ndama wanaweza kuyapata hasa wale ambao kwa mara ya
kwanza wanaachiwa kwenda nje kula nyasi kama vile ugonjwa wa mtoto wa jicho
ambao unaletwa na inzi ambao wanasambaza bacteria kutoka kwenye mifugo mingine
lakini pia katika kula wanakutana na minyoo ambayo baadae huwaletea viribatumbo
Amemalizia kwa kuwataka wafugaji kuwa na desturi ya kusafisha mazingira ya mifugo yao mara kwa mara hasa banda la mifugo kwa ufugaji endelevu na wenye tija.
0 Comments