SUAMEDIA

Mkuu wa Chuo Kikuu SUA aahidi kufanya kazi bega kwa bega na wanajumuiya wa Chuo hicho

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na wanajumuiya wa chuo hicho ili kuhakikisha chuo kinapiga hatua na kuendele kutatua changamoto katika kilimo hususani katika mazao yanayo zalisha mafuta ili kuondokana na changamoto ya uhaba wa mafuta nchini

Ameyasema hayo katika warsha ya utoaji taarifa ya utekelezaji wa mafanikio ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kipindi cha miaka mitano kwa mwaka 2017/2022. Iliyofanyika katika Kampasi Kuu ya Edward Moringe Sokoine Jaji Warioba ametoa shukrani kwa Serikali kwa kufanya kazi bega kwa bega na Chuo licha ya changamoto mbalimbali ikiwemo Covid 19 na kuupongeza utendaji kazi shirikishi wa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda pamoja na wafanyakazi wa jumuiya ya SUA kwa ujumla. Amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali chuoni hapo kwa kipindi hicho cha miaka mitano ni kutokana na bidii pamoja ushirikiano baina ya uongozi pamoja na wafanya kazi na hivyo basi malengo tarajiwa yanategemea ushirikiano huohuo kwa miakla mingine mitano.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Sayansi na Elimu ya Juu Mhe. James Mdoe ameupongeza uongozi wa chuo kwa kazi kubwa ambayo wameifanya kwa muda wa kipindi cha miaka mitano na kuwataka kufanya kazi kwa nguvu zaidi kutokana na kukua kwa teknolojia hivyo wanatakiwa kuhakikisha na maarifa ya kutosha kinadharia na vitendo.
Ameongeza kuwa katika malengo waliyoweka kwa kipindi cha miaka mitano mengine wapaswa kuwa na mikakati thabiti katika kuhakikisha wanaandaa mazingira rafiki ambayo yanaweza kukabiliana na idadi ya wanafunzi inayoongezeka kila mwaka na zaidi katika ufundishaji kwa vitendo ili kutoa wataalam waliobobea kwa njia ya nadharia na vitendo

Katika video

Post a Comment

0 Comments