SUAMEDIA

TMDA yaonya matumizi, uuzaji holela wa vidonge vya P2

 


Na Paul Yohana, Geita.

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imewataka vijana kuacha kuendekeza matumizi holela ya vidonge vya kudhibiti mimba maarufu kama P2 badala yake wafanye hivo kwa ulazima na kwa maelekezo ya daktari kuepuka madhara.

Aidha TMDA imewaonya wafanyabiashara wa maduka ya dawa muhimu kuachana na uuzaji holela wa vidonge hivo kwani sheria imeagiza vidonge hivo kuuzwa kwenye maduka maalumu yaliyo na wataalamu wa afya.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Magharibi Ofisi za Geita, Dk Edgar Mahundi wakati akifanya mahojiano maalumu na muungwana blog  ofisi kwake .

Dk Mahundi amesmea  TMDA imefanya msako kwenye maduka ya dawa muhimu katika mikoa ya Geita na Kagera na kubaini uuzaji holela wa vidonge vya P2 kwa asilimia takribani 40 na kudaka jumla ya pakiti 87 vya vidonge vya P2.

Ameeleza, TMDA wamekagua jumla ya maduka 81 mkoani Kagera na kubaini maduka 22 yakiuza vidonge vya P2 kiholelea huku jumla ya maduka 65 yamekaguliwa mkoani Geita, kati yake maduka 17 yalikutwa na vidonge hivo.

“Kwa wale ambao tumewakuta nazo hizi dawa, kwa mjibu wa sheria ya ada na tozo, ya mwaka 2021 ya TMDA kwanza hizi dawa tumeziondoa kwenye maduka husika, na hizi dawa zinaenda kurudishwa kwenye vituo vya kutolea huduma”.

Amesema, wahusika wamepewa onyo kali na kupewa katazo la kuuza dawa hizo na watakaokiuka watachukuliwa hatua za sheria ikiwemo kufungiwa maduka, kungang’anywa leseni na hata kupelekwa mahakamani.

 

Post a Comment

0 Comments