Na: Amina Hezron
Katika kuadhimisha Wiki ya Upandaji Miti Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesema kitapanda miti 18, 000 ya Mitiki katika eneo la Mafiga mkoani Morogoro ili
kuunga juhudi za serikali katika zoezi hilo.
Akizungumza na SUA Media Rasi wa Ndaki ya Misitu Wanyamapori
na Utalii Prof. Suzana Augustino amesema
kuwa lengo la kuchagua eneo hilo ni kutokana na aina ya miti yenyewe
itakayopandwa itastawi vizuri kwa eneo hilo.
“Menejimenti ya chuo ilishauri kwamba miti hiyo ipandwe katika
eneo kubwa ambalo baadae tunaweza kulitumia na wanafunzi wetu kwa mafunzo
kwahiyo mkakati wetu lile eneo tutapanda kwa kiasi kikubwa ambacho wanafunzi
wetu watakuwa wanalitumia kwa mafunzo haya ya muda mfupi wakiwa darasani wanatoka
kwenda kujifunza”, alisema Prof. Suzana.
Aidha Prof. Suzan amewataka wananchi kujitokeza kushiriki katika siku hiyo ya kupanda miti kwa kuwa
miti hiyo si kwa ajili ya mazingira tu ila pia kwa matumizi endelevu ya sasa na baadae.
“Wiki hii yote tunawakaribisha tunagawa miche bure miche ya
mikaratusi na tuna miche ya mijoholo ambayo tumeotesha pale, lakini pia tuna
mikangazi kwa watakao hitaji na mpaka sasa tumeshatoa miche zaidi ya 3000 kwa
watu ambao wameomba kwa ajili ya kupanda na sisi tumewapatia”, alisema Prof. Suzana.
0 Comments