SUAMEDIA

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando ameitaka SUA kurejesha Uoto wa Asili na kuondoa Hewa Ukaa


NA Gladness Mphuru

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro  Albert Msando amekitaka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kuisaidia wilaya na mkoa wa Morogoro  kurejesha uoto wa asili na kuondoa hewa ukaa  kwa kutumia Wataalamu hasa wa Misitu kutoka Chuoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro  Albert Msando akizungumza wakati akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martin Shigela kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Upandaji miti yaliyofanyika katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga manispaa ya Morogoro.

Msando ametoa kauli hiyo Machi 26, 2022 wakati akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martin Shigela kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Upandaji miti yaliyofanyika katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga manispaa ya Morogoro.

 “Na mimi nimefurahi kwa malengo yenu yote manne lakini yapo “internal” kwa ajili ya kufundisha, kulinda mipaka, kulinda ardhi yetu na kwaajili ya kupata kiwango kidogo katika mashamba yenu, haya yote ni kwa ajili ya SUA lakini tutoke na kuiangalia wilaya, tunaisaidia vipi wilaya yetu na mkoa wetu kwa kutumia utaalamu wenu” , amesema Msando.

Mkuu huyo wa wilaya amezitaka Taasisi nchini kupanda miti kama uzio na mipaka badala ya kujenga ukuta ili kupunguza gharama, sambamba na kuwaasa wanafunzi wa SUA hususan wanaosoma Misitu na Maendeleo ya Jamii wanapoenda kufanya masomo yao kwa vitendo wawapatie elimu wananchi ya utunzaji mazingira kupitia upandaji miti.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA Prof. Raphael Chibunda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala, Fedha na Mipango Prof. Amandus Muhairwa amesema Chuo pamoja na Misitu yake ya ndani pia kinamiliki misitu nje ya Morogoro, ikiwemo misitu ya Mazumbai yenye hekta 320 pamoja na hekta 10,000 katika wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma ambayo hadi sasa Chuo kimekwishapanda miti 1,200.

“Lengo la Chuo kila mwaka ni kupanda hekta 200 za miti ambapo msimu wa mwaka huu tumepata miti 400,000 ambayo ni maendeleo makubwa ukilinganisha na miaka iliyotangulia”, amesema Prof. Muhairwa.

Kwa upande wake Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyama Pori na Utalii SUA Prof. Suzana Agustino, amesema Chuo Kikuu cha SUA kwa kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais  Samia Suluhu Hassan kitahakikisha kuwa misitu inaongezeka na mazingira yanahifadhiwa na kutunzwa kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

“Zoezi hili limekuwa likifanyika kila mwaka, ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika uhifadhi wa Rasiliamali, Misitu na Mazingira kwa ujumla, na katika miaka yote hiyo tumebahatika kuwa na viongozi wa Chama na Serikali katika nyadhifa mbalimbali ambao walifika kuungana nasi katika zoezi la upandaji miti”, amesema Pfor. Suzana.

Wiki ya upandaji miti mwaka huu kitaifa ilizinduliwa rasmi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza, Machi 21 huku ikibeba Kauli mbiu isemayo “Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, Kazi iendelee”.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro  Albert Msando akipanda Mti katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga Manispaa ya Morogoro  kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Upandaji miti yaliyofanyika katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga manispaa ya Morogoro. 

 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala, Fedha na Mipango Prof. Amandus Muhairwa akipanda mti   kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Upandaji miti yaliyofanyika katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga manispaa ya Morogoro.
Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyama Pori na Utalii SUA Prof. Suzana Agustino ( kulia )aliposhiriki katika kupanda miti katika Maadhimisho ya Wiki ya Upandaji miti yaliyofanyika katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro  Albert Msando akimwagilia mti baada ya kupanda kwa ishara ya kuupa uhai akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martin Shigela kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Upandaji miti yaliyofanyika katika eneo la Chamwino mkabala na stendi ya Mafiga manispaa ya Morogoro.





KATIKA VIDEO



Post a Comment

0 Comments