BBC SWAHILI
John Nahimana anafundisha unyoaji nywele katika chuo kikuu cha Marekani, na alianza kazi yake katika kambi ya wakimbizi ya Kanemba nchini Tanzania kwa kutumia mkasi.
Nahimana anasema kwamba kunyoa kiutani alafu baadae akanufaika na kazi.
"Eti nilianza kunyoa kiutani alafu baadaye ilinisaidia kununua mafuta ya taa ili niweze kusoma alafu nikaweza kununua hata baiskeli kwendea shule," anasema.
"Wakati huo nilikuwa natumia mkasi mmoja."
John Nahimana aliondoka Tanzania na kuhamia kambi za wakimbizi katika nchi nyingine nyingi kama Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Afrika Kusini hapo pote alikuwa anafanya kazi ya kunyoa.
Mara nyingi alikuwa anafanya kazi na wenginr isipokuwa Afrika Kusini na Malawi alikuwa na 'saluni' yake.
Wakati wote huo alikuwa alikuwa anafanya kazi ya kunyoa huku anasoma.
"Niliporudi Malawi kutoka Afrika Kusini, ndipo niliponunua gari langu la kwanza kutoka kwenye kipato cha kunyoa.
Baadaye nilinunua la pili lakini sikuacha kufanya kazi hiyo.
Alipopata nafasi ya kwenda Marekani, haikuwa rahisi kwake kuendelea na kazi yake ya kunyoa.
Aliambiwa kuwa ili amiliki saluni yake binafsi anapaswa kuwa na cheti, anasema eti niliambiwa kwamba ili kuendelea kunyoa nchini Marekani napaswa kuwa na cheti.
Kwa kuwa nilikuwa nimetoka Afrika nikiwa na elimu ya kidato cha pili, nilianza kusoma kozi ya kunyoa chuo kikuu kwa muda wa mwaka mmoja.
Kwa vile nilitoka wa kwanza katika jimbo la idaho nchini Marekani, nilipewa kazi ya kufundisha kozi hiyo katika shule mbalimbali.
Kwa sasa naenda kusaidia kufundisha katika majimbo mbalimbali kama Arizona na Colorado.
John Nahimana alishatunukiwa tuzo mbalimbali.
Moja kama kinyozi bora katika jimbo analoishi mwaka 202, nyingine ya hivi karibuni alipewa na chuo kikuu cha Phoenix jimbo la Arizona mnamo tarehe 5, mwaka huu.




0 Comments