SUAMEDIA

Mzozo wa Ukraine: Bado kuna uwezekano wa shambulio la Urusi - Biden

CHANZO BBC

Joe

Shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine "bado lina uwezekano mkubwa wa kufanyika ", lakini garama ya kibinadamu ''itakuwa kubwa'', amesema Rais wa Marekani Joe Biden.

Katika hotuba yake ya kitaifa iliyotangazwa na televisheni kote nchini, Bw Biden alisema Marekani iko tayari kujibu kwa hatua ya haraka.

Rais huyo wa Marekani amesema kuwa Urusi sasa imerundika kiasi cha wanajeshi 150,000 kwenye mpaka wake na Ukraine.

Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema baadhi ya wanajeshi wameondoka. Bw Biden amesema kwamba hilo halijahakikishwa.

"[Kuondoka kwa vikosi vya Urusi] itakuwa vizuri , lakini bado hatujahakikisha hilo. Hatujahakikisha kuwa vikosi vya kijeshi vya Urusi vinarudi kwenye ngome zake za nyumbani ," rais wa Marekani alisema. "Kwa kweli, tathmini yetu inaonyesha kwamba bado wapo katika nafasi ya kutisha ."

Hotuba ya Biden inakuja saa kadhaa baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kuwa hofu za usalama za Urusi zinapaswa kutatuliwa na kuchukuliwa kwa umakini.

Bw Putin kila mara amekuwa akikana kuwa anapanga shambulio, na alisema Urusi haitaki vita nyingine katika Ulaya. Hatahivyo hali ya wasi wasi imekuwa ikiongezeka tangu mwezi wa Disemba.

Russia Ukraine map

Urusi ina uhusiano wa kitamaduni n awa kihistoria na Ukraine, ambayo ni Jamuhuri ya zamani ya Usovieti.

Bw Putin anataka hakikisho kwamba haitajiunga na Muungano wa kijeshi wan chi za magharibi -Nato, kwasababu anaona kupanuliwa kokote kwa maeneo Nato kama tisho kwa Urusi. Nato imepinga dai hilo.

Bw Biden alisema kuwa alikubaliana na pendekezo la serikali ya Urusi la kuendelea kwa diplomasia.

Rais wa Marekani pia ameonya kuwa uchumi wa Marekani unaweza kuvurugwa- kutokana na usambazaji wa nishati na mfumuko wa bei iwapo itatokea kwamba vikwazo vitawekwa dhidi ya Urusi katika kujibu uvamizi wowote wa Ukraine.

"Watu wa Marekani wanaelewa kulinda demokrasia na uhuru na havijawahi kupatikana bila garama ,"rais wa Marekani alisema. "Sitadanganyha kuwa hili halitaleta maumivu."

Alisema kuwa utawala unafanya juhudi kuandaa mipango na wazalishaji wa nishati na wasafirishaji ili kuondoa uwezekano wa tatizo la usambazaji wa nishati.

Bw Biden alionya kuwa pendekezo la Urusi la bomba la kujenga mtambo wa gesi wa - Nord Stream 2 unaokwenda hadi Ulaya "halitatekelezwa " iwapo uvamizi wa Ukraine utaendelea.

Rais wa Marekani aliendelea kusema kuwa: "Kwa raia wa Urusi: ninyi sio maadui zetu, na siamini mnataka umwagaji damu, vita vya uharibifu dhidi ya Ukraine."

Nato ilielezea "kuwa na Imani kidogo" Jumanne kuhusu tangazo la jesi la Urusi kwamba limeondoa baadhi ya vikosi vyake kutoka kwenye mpaka wa nchi hiyo na Ukraine.

Post a Comment

0 Comments