SUAMEDIA

Mataifa yanayozalisha mafuta kuamua kuhusu uzalishaji

 Mkutano wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani OPEC unafanyika leo kuamua kuhusu kiwango cha uzalishaji wa nishati hiyo kuanzia mwezi Januari chini ya kiwingu cha aina mpya ya kirusi cha corona kilichoyateteresha masoko duniani.



 OPEC pamoja na washirika wake wakioongozwa na Saudi Arabia na Urusi wanafanya mkutano huo kwa njia ya video wakati tayari wamekataa shinikizo la Marekani la kuongeza kiwango cha uzalishaji mafuta.

 Wafuatiliaji wa mkutano huo wanatabiri OPEC na washirika wake wataachana na uzalishaji wa nyongeza wa mapipa 400,000 kwa siku kila mwezi, uamuzi uliopitishwa mwezi Mei mwaka huu.

 Mataifa hayo yana wasiwasi kwamba kirusi kipya cha corona kitazidisha wasiwasi kwenye masoko ya mitaji na kupunguza mahitaji ya nishati ya mafuta na kuporomosha bei za nishati hiyo duniani.

Post a Comment

0 Comments