Na.Vedasto George.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuna kasumba ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wanje na kuweka urasimu mwingi kwa wawekezaji wandani.
Samia ameyasema hayo Mkoani Pwani wakati akizindua kiwanda cha Raddy Fiber ambacho ni cha nne kwa ukubwa Afrika kwa sasa lakini kitakapo kamilika ujenzi wake kitakuwa cha tatu Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua kazi mbalimbali katika kiwanda cha kutengeneza Nyaya za Mawasiliano cha Reddy Manufacturing Tanzania Limited kilichopo Mkuranga mkoani Pwani leo tarehe 03 Desemba,2021.
Rais Samia amesema kuchelewesha uwekezaji nchini ni kuchelewesha ajira kwa watu ambao wangeajiriwa katika viwanda husika pia uchelewesha mapato ya kodi ambayo Serikali inapata kwa viwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza Nyaya za Mawasiliano cha Reddy Manufacturing Tanzania Limited kilichopo Mkuranga mkoani Pwani leo tarehe 03 Desemba,2021.
0 Comments