Na Gladness Mphuru
SUA
Bonanza la michezo ya wafanyakazi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) maarufu kama Chibunda Cup 2021 limefungwa rasmi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, huku akipongeza menejimenti ya chuo, wafanyakazi pamoja na Benki ya CRDB na NMB kwa kudhamini mashindano hayo.
Pongezi hizo
zimetolewa tarehe 10, Decemba 2021 na Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga, wakati akihitimisha na
kufunga bonanza hilo la michezo katika viwanja vya Kampasi ya Edward Moringe
Sokoine Mkoani Morogoro
“Kwanza nichukue
nafasi hii kuwapongeza sana wale wote walioshiriki katika mashindano haya
inawezekana wameshiriki lakini hawakuwa washindi lakini kwangu mimi nasema
wamepata faida kubwa kushiriki mashindano haya na pia nichukue nafasi
kuwapongeza wadhamini wa mashindano
taasisi CRDB na NMB kwa huo ni mwanzo wa kuendelea kudhamini mashindano
hayo“ alisema Mhe. Kihanga
Aidha Mhe. Kihanga amesema Morogoro ina vipaji vingi na
SUA ni Taasisi ambayo inakusanya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini kupitia
michezo inayoendelea kuchezwa chuoni hapo itakuwa chachu ya kujenga timu imara
ya Chuo, itakayoleta hamasa, huku
akifurahishwa kuona Chuo kikikumbuka timu ya zamani ya SUA ambayo
iliweza kufika mbali katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa
Morogoro.
Awali
akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo Prof.
Raphael Chibunda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Maulid
Mwatawala, amesema kuwa bonanza hilo lilianza Oktoba 6 2021 ambapo michezo takribani
20 ilichezwa tofauti na miaka ya nyuma
Prof. Mwatawala
ameongeza kuwa dhima ya bonanza hilo ni kuwakutanisha wafanyakazi ili waweze
kufahamiana, kuimarisha afya zao, kuburudika na kuibua vipaji ambavyo husaidia
kufanya vizuri katika mashindano ambayo wanashiriki.
Aidha amesema
mbali na hayo Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Sua bado kinaendelea kuimarisha
miundombinu mbalimbali kwa viwanja vya michezo, ikiwemo kwa mchezo wa kriketi
na mpira wa tenisi.
“Wasomi wengi
Tanzania wameweza kupata fursa ya kusoma nchini marekani na nchi zingine
zilizoendelea hakika ushirikiano huu umesaidia kutoa fursa kwa vijana wetu na
umeongeza ukuaji wa uchumi nchini hivyo kwa kupitia hili tunajivunia sana’’
alisema Prof. Mwatawala
0 Comments