SUAMEDIA

Shughuli za kibinadamu sizizozingatia matumizi bora ya Ardhi chanzo cha kupotea Misitu ya asili

 

Na.Vedasto George

Imeelezwa kuwa kuwepo kwa Shughuli za kibinadamu sizizozingatia matumizi bora ya Ardhi nchini ndo chanzo kikubwa cha kupotea kwa misitu ya asili   na kuifanya dunia kubaki jangwa.

Hayo yameelezwa na Dkt.Felician Kilahama Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Msitaafu wakati akikabidhi vitabu Zaidi ya 100 vya kujifunzia ambavyo ni Mahususi kwa ajiri ya kutunza misitu na mazingira katika Ndaki ya Misitu,Wanyamapori na utalii ya  Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA.



Dkt.Felician Kilahama amasema   kwa sasa asilimia kubwa ya misitu ya asili inapotea kutokana   na kuwepo kwa shuguli za kibinadamu zisizo zingatia matumizi bora ya Aridhi.

Kwa upande wake Dkt. Eng Ibrahimu Mjema Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Mkuu wa Chuo na Menejimenti ya Chuo amesema chuo kina mpongeza na kumshukuru Dkt. Felician kilahama kwa kuwa ametambua mchango mkubwa unaotolewa katika jitihada za kuzalisha wataalamu wa misitu na kuongeza kuwa chuo kitahakikisha vitabu hivyo vinatumika kwa masilahi mapana ya Taifa.

Aidha Dkt. Eng.  Mjema amesema  ni muda sasa wa wataalamu wa Ndaki ya Misitu,Wanyamapori na utalii kutumia fursa  ya vitabu hivyo kusoma Zaidi na kuelewa jinsi gani misitu inaweza kutunzwa na kuhakikisha utaalamu wao unafika kwa jamii.

Naye Rasi wa Ndaki ya Misitu,Wanyamapori na Utalii Prof.Suzana Augustino amesema ndaki hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya uwepo wa vitabu vya kizamani ambavyo  mara nyingi vimekuwa vikilalamikiwa na wanafunzi wa Ndaki hiyo.

Ame sema ametengeneza historia kubwa kwenye  Ndaki hiyo ya Misitu,Wanyamapori na utalii kwa kutoa  hazina hii kubwa  kwani  wanayo  maktaba ndogo  moja na changamoto waliyonayo inavitabu vya kizamani na wanafunzi wamekuwa wakileta malalamiko  kwa Rasi wa Ndaki wakiomba vitabu, Maktaba yao ya Taifa imekuwa ikitusaidia  lakini  Chuo kinakuwa  na mahitaji  mengi  hata wanapoomba vitabu vinavyoletwa  kwa sekta ya Misitu,Wanyamapori na utalii sio vingi sana, Amesema Prof. suzana Augustino

KATIKA VIDEO


Post a Comment

0 Comments