SUAMEDIA

Simba na Mtibwa Sugar mambo magumu leo

 

 SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba ameweka wazi kuwa mchezo wao wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar ni mgumu kwa sababu wapinzani hao wamekuwa wakiwapa changamoto muda wote.



Uwanja wa Mkapa leo Aprili 14, Simba ambao ni mabingwa watetezi wana kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar inayopambana kujinasua kwenye nafasi ya kushuka daraja.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 imekusanya pointi 24 inakaribishwa na Simba iliyo nafasi ya tatu na ina pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

 Matola amesema kuwa hautakuwa mchezo mwepesi kwao ila watapambana kufanya vizuri.

"Mechi ngumu na Mtibwa Sugar hilo lipo wazi lakini mara nyingi Mtibwa wamekuwa wakitupa changamoto pale ambapo tunakutana.

"Tunahitaji pointi tatu muhimu hilo ndilo ambalo tumelifanyia kazi na wachezaji wanatambua jambo ambalo tunahitaji," .

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro timu hizo ziligawana pointi mojamoja baada ya sare ya kufungana bao 1-1.

 

Post a Comment

0 Comments