SUAMEDIA

Marekani kuhakikisha Iran haimiliki Nyuklia kamwe

 


Marekani imetangaza kuwa itafanyia kazi usalama wa Israel na "kuhakikisha kuwa Iran haimiliki silaha za nyuklia kamwe".

Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani Emily Horne alisema katika taarifa ya maandishi kwamba mkutano wa Ushauri cha Kimkakati cha Marekani na Israel ulifanyika chini ya mwenyekiti wa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani  Jake Sullivan.

Mkutano huo ulijadili mbinu za kuongeza utulivu na usalama .

Mkamu wa Rais Harris amesisitiza usalama wa Israel na kuhakikisha kuwa Iran haipati silaha za nyuklia kamwe.

Post a Comment

0 Comments