Kanye West amekubali kutunza
watoto wake wanne kwa ushirikiano na Kim Kardashian.
Hatua yake inafuatia
ombi la talaka lililowasilishwa na Kardashian tarehe 19 Februari, ambalo
lilianzisha mchakato wa kumaliza ndoa yao ya karibu miaka saba.
Katika maombi yao
wasanii hao wawili nyota, wamekubaliana kumaliza ndoa yao kufuatia tofauti ambazo
haziwezi kusuluhishwa.
Wamekubaliana kwamba
hakuna kati yao anayehitaji msaada wa mwenzake .
0 Comments