RWANDA
Serikali Rwanda imesema haitasitisha mpango wa kutoa chanjo
ya AstraZeneca.
Afisa mkuu Wa
mamlaka ya afya Dkt Sabin Nsabimana amewaambia waandishi wa habari mjini Kigali
kwamba chanjo ya Astrazeneca haina madhara.
Tangu wiki
mbili zilizopita Rwanda imeishatoa chanjo kwa watu wapatao laki mbili na
hamsini na saba elfu (257,000 ) ambapo zaidi ya theluthi mbili walipewa chanjo
ya AstraZeneca na wengine chanjo ya Pfizer.
Rwanda
inatarajia kupata dozi za chanjo ya corona milioni moja na tisini na nane elfu
miatisa sitini (1,098,960,) aina ya AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech,
zitatolewa kwa awamu wa kwanza na wa pili wa mwaka 2021.
0 Comments