SUAMEDIA

Upimaji wa Udongo unavyoleta tija katika kilimo endelevu

 Na: Tatyana Celestine.

Katika kuhakikisha mkulima anaachana na matumizi ya Teknolojia za mazoea hasa katika kilimo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimehakikisha mkulima, mwanafunzi anayetaka kujiunga na  chuo hicho wanapata uelewa katika kufahamu kuhusu umuhimu wa upimaji udongo kwa maendeleo ya kilimo nchini.



Hayo yamesemwa Septemba 3,2020 na Mtaalamu wa Sayansi ya Udongo na mimea kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  Bw. Stevenson Pelegy Noah kwenye Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayondelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo Chuo Kikuu cha Sokoine kipo kwa ajili ya kutoa ushauri wa kozi mbalimbali katika kujiunga na chuo, pia kudaili wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho.


Ameleleza kuwa kilimo kimeonekana kina changangamoto kubwa hasa kwa Wakulima ambao hawafuati njia bora katika hatua za ulimaji mazao mbalimbali hasa katika afya ya udongo katika mashamba yao ambapo imesababisha  wakulima wengi kuona mazao yao hayana tija ukilinganisha na kipato wanachopata.


Noah amesema Kitengo cha Sayansi ya Udongo na Mimea SUA kinahusika na kutambua hali ya afya ya udongo kabla ya kupanda kitu chochote kwa kufanya utafiti na kutambua zao lipi litafaa katika kilimo pamoja na kutambua  udongo huo una virutubishi vya aina gani kwa matokeo chanya.

 

Aidha amesema kuwa wakulima wanapopima udongo na kutambua hali halisi ya udongo huo hasa katika virutubisho itawasaidia kujua nini kilichopo katika udongo hii ikijumuisha matatizo,  udhaifu na uwingi wa viritubisho katika udongo ili viendelee kubaki katika hali inayohitajika

Katika hatua nyingine amewataka wakulima kuwatumia maafisa ugani au mabwana shamba ili kuwasaidia kutambua hali halisi ya udongo ambapo maafisa hao wapo katika maeneo mbalimbali nchini mbali na kusafiri na kwenda SUA kama ni mbali na eneo alipo.


Vilevile ametaja jinsi ya kuweza kutambua aina ya udongo katika shamba la mkulima kabla ya kumuona mtaalam hii itasaidia kumfanya aende kutafuta msaada wa upimaji udongo ili kujua anaweza kulima zao lipi katika aina ya udongo uliogundulika.


Amewataka vijana kuacha kuwasikiliza wanaosema kujiunga na Chuo Kikuu cha SUA kuwa  kuna ugumu hivyo kutokata tamaa na watambue kila kinachosemwa kina ugumu kuwa kina mafanikio kwani mwanafunzi anayemaliza chuo kikuu cha sokoine anakuwa bora na thamani katika soko la ajira nchini

KATIKA PICHA








Post a Comment

0 Comments