SUAMEDIA

SUA kufuatilia Wanafunzi katika mafunzo kwa vitendo ili kukidhi Soko la Ajira

 

Na: Tatyana Celestine.

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA pamoja na kuendelea  kutoa elimu inayomfanya mwanafunzi awe mzuri katia Soko la ajira Chuo hicho kimedhamiria kuwasimamia vema wanafunzi ili waweze kupata ujuzi zaidi kwa vitendo kwa kuanzisha mfumo imara wa ufuatiliaji wawapo katika mafunzo yao kwa vitendo


Akizungumza katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Shahada za Awali Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dkt. Nyambilila Amuri amesema maonesho ya TCU yamekuwa fursa nzuri ya kuwafanya wahitimu wa Diploma na Kidato cha sita kufahamu Program zitolewazo SUA na jinsi ziavyoendeshwa ambazo ni tofauti na vyuo vingine nchini.


Dkt Amori amesema kuwa chuo kinahakikisha wanafunzi watokao SUA wanaweza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini kwa weledi mkubwa na ndio maana chuo kimeamua kuandaa mpango wa kuwafuatilia kwa ukaribu hasa wawapo katika mafunzo kwa vitendo ili wataalammu hao waweze kusaidia kufanya sekta ya kilimo iende mbele.


Amesema Chuo cha SUA kina uzoefu mkubwa katika masuala ya Kilimo, utunzaji wa rasilimali, maliasili pamoja na uchumi kilimo hivyo chuo kinaendelea kupokea wanafunzi waliosoma masomo mbalimbali bila kujali mchepuo ambao mwanafunzi alisomea hapo awali kinachotakiwa  awe amekidhi vigezo vya kozi anayotaka kusomea

Ameongeza kuwa SUA imeendelea kupanuka ambapo pia wanafunzi wanapokelewa  kwenye Kampasi mpya ya Mizengo Pinda iliyopo Katavi nayo inaanza kutoa Program tatu mpya ambazo ni kozi za Shahada ya Rasilimali Nyuki, Stashada ya Kilimo cha Mazao, Astashada ya Uongozaji Watalii na shughuli za Uwindaji.


Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wanafunzi na wazazi watumie kipindi hiki cha maonesho hayo ya vyuo vikuu kuweza kufika katika banda la SUA kupata muongozo na ushauri kwa kujiunga na chuo, kusajili wanafunzi, kupata taarifa za kozi mbalimbali,pia kupata taarifa nyingine mbalimbali zinazohusu Chuo Kikuu cha Kokoine cha Kilimo SUA hasa kwa wale ambao hawajui nini kinapatikana SUA.


Maonesho hayo yameanza Agost 31 na kutarajia kumalizika Septemba 5, 2020 yakiwa yamebebwa na kauli mbiu isemayo Nafasi ya Elimu ya juu Katika Kuleta Mabadiliko ya Kiuchumi ya Maendeleo Endelevu.







Post a Comment

0 Comments