SUAMEDIA

Wakulima washauliwa kutumia mbinu bora za kilimo zinzoweza kutunza mazingira.

 

Na.Vedasto George.

Wakulima na wafugaji nchini wameshauliwa kutumia mbinu bora za kilimo zinzoweza  kutunza mazingira ili  kizazi cha sasa na kijacho kiweze kunufaika na kilimo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.


Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitalaamu Prof. Erson Karimuribo aliyekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa ICE Prof. Mwaseba na kushoto ni Prof. Sibuga

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitalaamu Prof. Erson Karimuribo kutoka  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati akifungua warsha wa siku mbili ulio wakutanisha wadau mbalimbali  wa kilimo, wanafunzi wa SUA, Wataalamu kutoka mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali ya ikolojia pamoja na  wanafunzi kutoka chuo cha Nelsoni Mandela  kwa ajili ya kuchangia na kubadilishana uelewa wa namna ya kuendeleza kilimo ikolojia Tanzania.




 “Kilimo Ikolojia imekuwa ni dhana mpya kwa ajiri ya kuendeleza kilimo  kwa sababu ya mazingira siku za zamani kilimo chetu kilikuwa kinafuata taratibu bila ya kujali mazingira lakini sasa ivi tumeunganisha hizi tasinia mbili kilimo halisi pamoja na dhana nzima ya ikolojia ambayo inajali mazingira”Amesema Prof. Karimuribo

Aidha Prof. Karimuribo amesema kutokana  na changamoto ya uaribifu wa mazingira uliopo nchini kwa sasa  kilimo ikolojia kitasaidia kutunza mazingira Zaidi ya miaka 50 ijayo na kupunguza athari kwa wananchi.

 Tumeanza na mikoa ambayo inatuzunguka pamoja na wilaya zetu za mkoa wa Morogoro ambazo ni Mvomero pamoja na wilaya ya Morogoro mjini kwa sababu tunaona ni muhimu, pia tuna mkoa wa Mbeya,Arusha” Amesema Prof. Karimuribo

Kwaupande wake Mratibu  wa Mradi wa Kilimo Ikolojia Tanzania SUA, ambaye pia ni Mhadhili Mwandamizi kutoka Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA amesema lengo la mradi huo ni kufanya mageuzi katika kilimo, kuboresha Maisha ya mtanzania na  kuifadhi mazingiara 

Kupitia huu mradi tunategemea  kuongeza rasilimali watu kwa maana ya  kupitia mafunzo shahada ya juu ya uzamivu na uzamili na pia inatoa fursa kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza kufanya utafiti chini ya mradi  lakini mwisho wa siku tukipata tafiti hizo tuweze kuzisambaza kwa wakulima”Alisema Prof Mwaseba .

Naye Prof.  Kalunde Sibuga kutoka Idara ya Mimea Vipando na kilimo cha Busitani na kiongozi katika Mradi wa uimarishaji wa Vyuo Vikuu  unaoshirikiana na Mradi wa Kilimo Ikolojia amesema lengo la mashirikiao hayo ni kujenga kuwajengea uwezo wataalamu watakaofanya utafiti na kutengeneza Teknolojia zitakazotumiwa mashambani.

Mradi  wa Kilimo Ikolojia Tanzania Katika Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha kilimo SUA unafadhiliwa na mradi wa Mc Knigth wenye makao yake makuu nchini Marekani

Post a Comment

0 Comments