Na Mariam Mwayela
Arusha
Jaji Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Othuman Chande amekitaka kituo cha mafunzo ya misitu Olmotonyi mkoani Arusha kutumia misitu kufanya utalii kutokana na kuhamia kwa wanyamapori kutoka katika hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Wajumbe wa Baraza la chuo wakiwa katika msitu wa Olmotonyi
Jaji Mstaafu Chande akizungumza wakati wa ziara ya wajumbe wa Baraza la chuo hicho wakati wakitembelea kituo cha mafunzo ya msitu Olmotonyi amesema kwa kufanya hivyo kituo kitaweza kujiendesha bila kutegemea misaada.
"Hii itasaidia chuo kujiendesha kifedha na kuwa na mipango na uzalishaji mali, tunayo miradi yetu ndani ya chuo ya kuzalisha fedha zaidi na moja katika ni suala za kuweza kufanya utalii"
Kituo cha mafunzo ya msitu wa Olmotonyi hushirikiana kwa karibu na jamii inayo wazunguka kwa kufanya shughuli za kilimo kisicho kuwa na madhara katika misitu huku mipango ya kituo hicho ikiwa ni kuanzisha shughuli za utalii wa asili
Akizungumza malengo ya chuo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema wanataka kuona chuo kinajitegemea kwa kutengeneza mapato ya kutosha
"Kupitia msitu huu wa hifadhi tunaweza kufanya huu utalii asilia na hayo ni malengo yetu ya siku zijazo, lakini pia tunataka kuhakikisha chuo kinajiotegemea kwa kuwa na mapato" amesema Prof. Chibunda
Kwa upande wao Wanafunzi wa chuo hicho wamesema kituo kinawasaidia kupata ujuzi utakao isaidia jamii katika kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na misitu
0 Comments