Na Ayoub Mwigune
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeandaa Semina kwa ajili ya mafunzo kwa Wasindikaji wa vyakula mbalimbali kutoka manispaa ya Morogoro yenye lengo la kuhakikisha kazi mbalimbali za kitafiti na kiteknolija za Chuo hicho zinawafikia Watu mbalimbali katika Jamii.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mafunzo kutoka kwa mwezeshaji hayupo pichani
Akifungua Semina hiyo Chuoni hapo Prof. Esron Karimuribo ambaye ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ,Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam kutoka SUA amesema lengo la semina hiyo ni kuhakikisha kuwa kazi za Kitafiti zinazofanywa na Chuo hicho zinawafikia Wakulima
Naye Dk. Doreen Ndossi ambaye ni Mratibu wa Mhaulishaji wa Teknolojia kutoka SUA amesema Chuo hicho kimeanzisha kitengo cha Teknolojia kinachofahamika kwa jina SUA Innovatiation Hub ambacho kina lengo la kuhakikisha kila Teknolijia na Ubunifu unawafika Walengwa katika Jamii
Kwa upande wake Dkt. Beatrice Kilima ambaye ni mhadhiri, Idara ya Teknolojia ya Chakula, Llishe na Sayansi ya Mlaji na Muwezeshaji katika Semina hiyo amesema mafunzo hayo yanawajengea uwezo Wajasiriamali katika Kuzalisha Vyakula ambavyo vitakuwa na ubora na usalama kwa ajili ya afya ya Walaji pamoja kanuni bora za usafirishaji wa Chakula na jinsi ya kuweza kupata nembo ya ubora kutoka TBS
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika mjadala
Bw.Ibrahim Diwani pamoja na Monica Yohana kwa pamoja wamesema Mafunzo hayo yamewafunza namna ya kuzingatia usafi wakati wa uzalishaji ,namna ya kuzalisha Bidhaa bora pamoja na kuweza kuingia katika ushindani wa soko .
0 Comments