SUAMEDIA

Mabadiriko ya tabianchi yasababisha kukosekana kwa chakula cha kutosha, na kusababisha wanaume wengi kuvunja ndoa zao na kutelekeza familia kwa kisingizio cha kwenda kutafuta chakula.

 Na.Vedasto George.

Imeelezwa kuwa kuwepo kwa mabadiriko ya tabianchi kumesababisha kukosekana kwa chakula cha kutosha,  na kusababisha wanaume wengi kuvunja ndoa zao na kutelekeza familia kwa kisingizio cha kwenda kutafuta chakula kitakacho weza kidhi maitaji ya familia.  

Mkurugenzi wa sera na Mipango OBADIAH NYAGIRO kutoka Wizara ya Kilimo Akifungua   kikao cha siku mbili cha jukwaa la wadau wa kilimo kinacho himili mabadiliko ya tabianchi kinacho fanyika mkoani Morogoro.picha na Vedasto George.

Akifungua  kikao cha siku mbili cha jukwaa la wadau wa kilimo kinacho himili mabadiliko ya tabianchi kinacho fanyika mkoani Morogoro kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mkurugenzi wa sera na Mipango OBADIAH NYAGIRO amesema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) ya mwaka 2018 imebainisha kuwa kaya zinapo kosa chakula cha kutosha kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi wanawake na Watoto ndio wanathirika Zaidi kuliko wanaume.


wito kwa wadau wote  sekita ya umma,sekta binafsi na wadau wa maendeleo kuhakikisha kwamba mbini na teknolojia za kilimo zinatumika katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinzzingztia Zaidi ushiriki wa wanawake na vijana,Ushiriki huo utatoa nafasi kwa kundi hili muhimu kushiriki katika kupanga na kupokea mipango na kuitekeleza hivyo kupanua kilimo himilivu katika nchi.amesema NYAGILO

 

Awali akimkaribisha mgeni rasimi Mwenyekiti wa jukwaa  la wadau wa kilimo kinachpo himili mabadiliko ya tabianchi TCSAA Stephano Kingazi amesema TCSAA imeanzisha kwa ajiri ya kupambana na kuona namna gani wanaweza kupambana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ikiwa na  kuleta majawabu chanya kwa wakulima ili kumfanya mkulima aweze kufanya kilimo chenye tija.


Mwenyekiti wa jukwaa  la wadau wa kilimo kinacho himili mabadiliko ya tabianchi TCSAA Stephano Kingazi akizungumza jambo na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kikao cha siku mbili cha jukwaa la wadau wa kilimo kinacho himili mabadiliko ya tabianchi. picha na Vedasto George. 

Lovina Japhet ni miongoni mwa washiriki katika jukwaa hilo la wadau wa kilimo kinacho himili mabadiliko ya tabianchi  na mtaalamu wa Mamlaka  ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kutoka Dar salaam ameeleza nafasi ya mamlaka hiyo katika kuakikisha mkulima kilicho bora.

Post a Comment

0 Comments