Na.Ayoubu Mwigune
Wajasiriamali na Wasindikaji wa Vyakula mbalimbali kutoka Manispaa ya Morogoro wamekishukuru Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa mafunzo ya usindikaji wa vyakula.
Wakitoa maneno ya shukurani katika kuhitimisha mafunzo hayo ya siku mbili, Bi Esther Muffui, Joyce Edwin pamoja na Ramadhan Sigaleti wamesema mafunzo hayo yamewanufaisha hasanamna ya kupata nembo ya ubora kutoka katika shirika la viwango nchini tanzania TBS jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwao
Wamesema kuwa watakuwa mabalozi wazuri kwa taaluma waliyojengewa na Chuo hicho wakibainisha kuwa watazidisha ufanisi ili kuweza kulifikia soko la kimataifa
Kwa upande wake Bi. Nuria Majaliwa mhadhiri, Idara ya Teknolojia ya Chakula, Lishe na Sayansi ya Mlaji ambaye pia alikuwa Mwezeshaji katika Semina hiyo amesema dhumuni la mafunzo hayo nikuwapa elimu na kupanua wigo wao wa biashara ili kuzalisha bidhaa bora na salama huku akiwaomba kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameweza kupata kupitia semina hiyo
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeandaa Semina kwaajili ya mafunzo kwa Wasindikaji wa vyakula mbalimbali kutoka manispaa ya Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kazi mbalimbali za kitafiti na kiteknolija za Chuo hicho zinawafikia Watu mbalimbali katika Jamii mafunzo ambayo yamehitimishwa leo hii.
0 Comments