Waislamu wasiopindukia 10,000 ambao tayari wanaishi nchini Saudi Arabia ndiyo watashiriki Hijja inayofanyika kwa siku tano, idadi ambayo ni sehemu ndogo ya mahujaji milioni 2.5 waliohudhuria mwaka uliopita.
Vyombo vya Habari vya Taifa vimeonesha wafanyakazi wa afya wakipuliza dawa ya kupambana na virusi kwenye masanduku ya mahujaji huku wengine wakipatiwa mikanda maalum ya kufuatilia mahali waliko.Kwa lengo pia la kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, mamlaka inayosimamia ibada ya Hijja pia imepiga marufuku kwa mahujaji kuligusa ´´Ka´bah´´ jengo dogo la mraba lililo katikati ya msikiti mkuu wa mjini Makka.
0 Comments