Na Mary Mwakapenda- Masasi
Hayati Benjamin William Mkapa wakati wa utawala wake pamoja na mambo mengine
aliyoyafanya kwa manufaa ya Taifa, atakumbumbukwa na watanzania kwa kuchukia
rushwa na umaskini na hatimaye kuanzisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ambapo
kwa kiwango kikubwa TAKUKURU imesaidia kupambana na Rushwa wakati
TASAF na MKURABITA zimeboresha maisha ya wananchi wenye kipato cha chini.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Huruma Mkuchika (Mb) kijijini Lupaso-Masasi alipokuwa akikagua maandalizi ya sehemu ambayo mwili wa Hayati Mkapa utapumzishwa.
Akifafanua kwa undani sababu za Hayati Mkapa kuanzisha Taasisi hizo, Mhe.
Mkuchika amesema kuwa, alichukia sana rushwa, hivyo alimteua Mhe. Jaji Joseph
Sinde Warioba kufanya utafiti ili kujua sababu za rushwa, mianya ya rushwa na nini
kifanyike kuzuia rushwa nchini na matokeo ya utafiti huo yakawa ni chachu ya
kuanzisha na kuimarishwa kwa TAKUKURU.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, Hayati Mkapa alichukia sana umasikini na
aligundua kwamba Watanzania wengi waliishi maisha duni ya mlo mmoja kwa siku,
hivyo aliwasisitiza wananchi kupambana na umaskini na kwa huruma yake alianzisha
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuzisaidia kaya maskini, Mfuko ambao
uliendelezwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
na sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli ambaye hivi karibuni alizindua Sehemu ya Pili ya Awamu ya Tatu
ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Aidha, amesema, Hayati Mkapa alianzisha MKURABITA ili wananchi wapate Hati za
Hatimiliki za Kimila zinazotolewa kwa Mujibu wa Sheria Na. 5 ya Ardhi ya Vijiji ya
Mwaka 1999 ambazo zinawawezesha kujipatia mikopo kwenye taasisi za kifedha
na kujikwamua kiuchumi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alifariki dunia
tarehe 23/07/2020 na anazikwa leo Kijijini kwake Lupaso-Masasi, Mkoani Mtwara.

0 Comments