Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema wakulima na wizara
yake imempoteza kiongozi ambaye si tu kwamba alisisitiza watanzania
kutumia nguvu zao kama mtaji katika kufanya kazi bali aliyehakikisha
kilimo kinatoa mchango mkubwa katika maendeleo yao na taifa kwa
ujumla.
Akizungumza kwenye maonesho ya kilimo biashara yaliyofanyika
kwenye Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Jijini Arusha
Mhe. Hasunga amesema kuna mambo mengi yakujivunia leo kwenye
kilimo ambayo yametokana na mchango mkubwa wa Rais wa awamu
ya tatu Hayati Mhe. Benjamin William Mkapa.
yake imempoteza kiongozi ambaye si tu kwamba alisisitiza watanzania
kutumia nguvu zao kama mtaji katika kufanya kazi bali aliyehakikisha
kilimo kinatoa mchango mkubwa katika maendeleo yao na taifa kwa
ujumla.
Akizungumza kwenye maonesho ya kilimo biashara yaliyofanyika
kwenye Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Jijini Arusha
Mhe. Hasunga amesema kuna mambo mengi yakujivunia leo kwenye
kilimo ambayo yametokana na mchango mkubwa wa Rais wa awamu
ya tatu Hayati Mhe. Benjamin William Mkapa.
Akizungumzia baadhi ya mambo hayo amesema ni msimamo wake
thabiti katika kuhakikisha wataalamu wa Kilimo kwa ngazi zote
wanatoka maofisini na kwenda kutoa Silima stahiki kwa wakulima na wafugaji ili kilimo kinachotegemewa na
zaidi ya asilimia 75 ya watanzania kitoe mchango unaostahili.
“Aliposema mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe alisisitiza
watu kutumia nguvu zao kama mtaji katika uzalishaji mali kwa
kufanya kazi mbalimbali hasa za kilimo ili kutokomeza njaa na
umasikini kwenye kaya”, alisema Mhe. Hasunga.
Waziri huyo wa Kilimo pia alibainisha kuwa uanzishwaji wa TASAF
ilikuwa ni moja ya jitihada za kusaidia kaya masikini ambazo nyingi
zipo vijijini zinajishughulisha na kilimo huku akipambana na rushwa
kwa kuanzisha Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU
ili masikini wapate haki kwenye ofisi za serikali na kwenye maeneo
mengine wanapokwenda kutafuta huduma.
“ Niwatakie watanzania hasa wakulima na wataalamu wa kilimo
kumuenzi kwa vitendo marehemu Benjamin Mkapa kwa yake
yote ambayo aliyaanzisha na kuyasisitiza ili kuwakomboa
watanzania wanyonge na wale wenye kipato cha chini”, alisisitiza
Mhe. Hasunga.
Waziri huyo wa Kilimo pia ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania TARI na Kituo cha Utafiti cha Selian cha Jijini Arusha kwa
kuandaa maonesho hayo ya Kilimo Biashara kwa lengo la kuwezesha
wakulima kujionea na kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa za
kilimo ili ziwasaidie kuboresha kilimo chao na kuongeza tija.
Amesema kilimo cha kizamani na cha kutumia mbegu za asili hakina
tija kwa mtazamo wa kibiashara na badala yake watumie mbegu
zilizoboreshwa ili wazalishe zaidi na kupata ziada lakini serikali
haizuii wakulima kulima mbegu za asili lakini tafiti zinaonesha
mbegu za asili hazina tija sana kutokana na uwezo wake wa kushindwa
kuhimili magonjwa, wadudu na mabadiliko ya tabia nchi.
Awali akieleza malengo ya maonesho hayo Mkurugenzi wa Kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Jijini Arusha ambao ndio walioandaa
maonesho hayo Dkt. Joseph Ndunguru amesema ni kuwaonesha
wadau wote wa kilimo teknolojia, Mbinu na aina mbalimbali za mbegu
ambazo wamezalisha ili wakulima wazione na kuchagua zinazowafaa
kwenye maeneo yao.
Amesema kituo hicho ambacho kina dhamana kwenye utafiti wa
maharage kimezalisha mbegu mbalimbali za maharage ambayo yana
sifa ambazo ni kuvumilia magonjwa, zenye viinilishe mbalimbali hasa
madini ya chuma, zinazoendana na mabadiliko ya tabianchi pamoja
na zinazofaa kwa usindikaji kutimiza ndoto ya Tanzania ya Viwanda.
Dkt. Ndunguru amesema pamoja na kuonesha kazi zinazofanywa na
kituo hicho pia wametoa nafasi kwa wadau wengine wa kilimo hasa
makampuni ya mbegu na pembejeo zingine kuonesha bidhaa
wanazozalisha ili wananchi wapate uwanja zaidi wa kuchagua
kulingana na mahitaji yao ya kilimo kwenye maeneo yao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt. Geofrey Mkamilo amesema
taasisi yake ina vituo 17 nchi nzima ambavyo vinafanya kazi kubwa ya
kuzalisha teknolojia mbalimbali kulingana na mahitaji ya kanda husika
za kilimo na kwamba kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuhakikisha
matokeo hayo mazuri ya utafiti kwenye kila kituo yanawafikia wadau
wote wa kilimo ili wazitumie na kuongeza uzalishaji.
“ Niwatamkie rasmi leo waandishi wa habari wa vyombo
mbalimbali nchini nyie ni sehemu ya TARI na naomba
wakurugenzi wote wa vituo kokote nchini kufanya kazi na
waandishi wa habari ili wasaidie kufikisha matunda ya tafiti zetu
kwa jamii kwa upana wake maana hatuwezi kufika kila mahali kama ambavyo vyombo vya habari vinafika”, alisisitiza Dkt. Mkamilo.
Aidha Mkurugenzi huyo Mkuu wa TARI amesema kuwa hivi sasa
wameanzisha utaratibu mzuri ambao vituo vyote vya utafiti vitakuwa
vinashamba la maonesho kwenye vituo vyao kuonesha teknolojia
mbalimbali wanazozalisha kwa mwaka mzima ili wananchi wakaone
na kujifunza badala ya kutegemea wakati wa maonesho ya nanenane
pekee ambayo hufanyika siku nane tuu kwa mwaka.
Nao baadhi ya wakulima walioshiriki kwenye maonesho hayo ya
Kilimo Biashara wamemuomba waziri wa kilimo kusaidia somo la
kilimo kuanza kufundishwa kuanzia shule za msingi ili wale
wanaoshindwa kuendelea na elimu ya juu washiriki kwenye Kilimo
kwa kulima Kisasa.
0 Comments