Calvin Gwabara
Dar es Salaam
Wataalamu wa masuala ya Menejimenti ya Maarifa na Maafisa Mawasiliano nchini wametakiwa kuamka kutafuta maarifa hayo kutoka kwenye maeneo mbalimbali yanakozalishwa na kuyafikisha kwa jamii ili yakajibu changamoto zinazoikabili jamii katika kukuza uchumi wao na Taifa.
Mshauri namwezeshaji wa kimataifa Bwana Martin Muchero akileza na kufafanua maana ya Maazimio ya Malabo na yanavyotekelezwa kila nchi Mwananchama. |
Wito huo umetolewa na Meneja wa Mawasiliano na
Menejimenti ya Maarifa kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Dkt. Richard
Kasuga wakati akiwasilisha mada yake kuhusu Menejimenti ya Maarifa nchini hasa
katika sekta ya kilimo kwa maafisa menejimenti ya maarifa na mawasiliano kutoka
katika taasisi mbalimbali za utafiti, vyuo vikuu na maeneo mengine.
“Maarifa yapo mengi sana kwenye vituo vyetu vya
utafiti,vyuo vikuu na maeneo mengine yanayozalisha maarifa lakini jamii yetu
hasa wakulima hawawezi kufika kuzifuata na kuzitafuta huko lakini sisi kama
wataalamu wa menejimenti ya maarifa tunaweza kwenda kuzichimbua na kuwaletea
wananchi wetu kuzitumia na kubadilisha maisha yao. Alisema Dkt. Kasuga.
Dkt. Kasuga amesema kwenye kurasa za taasisi
mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia Mkulima Library,
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI, TARIRI, Mamlaka ya Hali ya Hewa,
NIMRI na nyingine nyingi kumewekwa maarifa mbalimbali wanayozalisha ambayo
yanahitajika na wakulima na wafugaji hivyo ni jukumu la wataalamu hao wa
mawasiliano na menejimenti ya maarifa kuzitembelea na kuchukua yanayohitajika
ili jamii ikayatumie.
Meneja huyo wa menejimenti ya maarifa na mawasiliano
wa TARI ameongeza kuwa siku hizi zipo njia nyingi za kufikisha maarifa kwa
jamii ambazo jamii inazitumie ikiwemo mitandao ya kijamii,kama vile twitter, facebook,
Instagram lakini pia Televisheni, Redio na Magazeti ambazo wanaweza kuzitumia
kufikisha elimu kwa walengwa kirahisi.
Tanzania inaendesha
mafunzo ya kitaifa ya siku nne ya
kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano, Wagani na Waandishi wa Habari namna ya
kuchakata matokeo ya Tafiti na kuwafikishia walengwa sambamba na kufuatilia na
kutoa taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Malabo ulioandaliwa na Taasisi ya
Uratibu wa Tafiti za Kilimo (CCARDESA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti
wa Kilimo Tanzania (TARI).
Bwana Shadrack Ndalawa msimamizi wa dawati la CAADP Wizara ya Kilimo akieleza utekeeleaji wa maazimio Malabo upande wa Tanzania.
Afisa Habari na Menejiment ya Maarifa kutoka kutoka Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo Afrika (CCARDESA) Bi. Bridget Kakulwa akieleza akieleza matarajio ya Mafunzo hayo. |
Afisa Programu ya CAADP -XP4, Bi. Futh Magagula akitoa salamu za Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo Afrika (CCARDESA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es salaam.
Meneja wa Kituo cha Utafiti cha TARI Mikocheni Dkt.Joseph Ndunguru akifungua mafunzo hayo ya kitaifa ya siku nne kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TARI.
0 Comments