SUAMEDIA

VIONGOZI WAPYA WA SUASA WATAKIWA KUZINGATIA NIDHAMU NA MAADILI YA KATIBA



Na, Ngolo Mboje

Viongozi wapya wa Chama cha Wahadhiri na Wafanyakazi wa Kitaaluma wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUASA) wametakiwa kuzingatia nidhamu, kusimamia katiba ya chama hicho na kuzingatia misingi na maadili yaliyowekwa kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama.            

Wito huo umetolewa na Profesa Maulidi Mwatawala, aliyemwakilisha mgeni rasmi, Profesa Rafael Chibunda Makamu Mkuu Wa Chuo cha sokoine cha kilimo Sua wakati wa hafla ya kuapishwa kwa viongozi wapya wa SUASA iliyofanyika katika Kampasi ya Edward Moringe ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mwatawala amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuimarisha umoja na kurejesha mshikamano miongoni mwa wanachama ili kuhakikisha chama kinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

“Ninaamini timu mpya itaendeleza hatua nzuri zilizofikiwa, kwa sababu uzoefu na maendeleo yaliyopatikana yataendelea kuwa na umuhimu mkubwa,” amesema Profesa Mwatawala.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya SUASA, Profesa Baanda Salim, amesema uchaguzi huo ulifanyika kwa kuzingatia katiba, kanuni na miongozo ya chama, huku akisisitiza kuwa ulikuwa huru na wa haki kwa wagombea wote.

Prof Salim Amesema ana imani kuwa uongozi mpya utaunganisha wanachama, kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha kila mwanachama anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama.

Naye Mwenyekiti mpya wa SUASA, Profesa Nsajigwa Mbije, ameipongeza Kamati ya Uchaguzi kwa kusimamia mchakato wa uchaguzi na kuahidi










Post a Comment

0 Comments