Na: Mwandishi wetu
Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) kimeendelea kuimarisha nafasi yake katika ulimwengu wa kitaaluma.
Kwa mujibu wa AD Scientific Index, SUA imeorodheshwa katika nafasi ya kwanza
Tanzania, ya 44 barani Afrika na ya 1,595 duniani kwa kuzingatia jumla ya
H-index, kiashiria kinachopima tija na athari za machapisho ya kitaaluma
kupitia nukuu za tafiti.
Mafanikio haya yanaakisi mchango wa watafiti wa SUA katika kuzalisha maarifa na kutatua changamoto za jamii, hususan katika sekta za kilimo, mifugo, misitu, afya na usalama wa chakula.
Aidha, mafanikio hayo yanatoa
hamasa kwa wanataaluma na watafiti kuendelea kufanya utafiti bora, kukuza
ubunifu na kuongeza mwonekano wa machapisho ya Chuo katika ngazi ya kimataifa.
Hongera SUA na watafiti wote
kwa mchango wenu katika kuendeleza sayansi na maendeleo ya Tanzania. Tuendelee
kufanya utafiti wenye matokeo chanya kwa jamii na kuimarisha nafasi ya SUA
barani Afrika na duniani.

0 Comments