SUAMEDIA

SUA yaanza hatua za kukabiliana na athari za mvua za El Niño

 Na: mwandishi wetu

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeanza kuchimba na kutanua Mto Ngerengere unaopita katika Kampasi ya Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu, Morogoro, ikiwa ni hatua ya tahadhari katika kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuchukua hatua za mapema katika kukabiliana na athari za mvua hizo. Utekelezaji huo unafanywa kupitia Kurugenzi ya Miliki na Ujenzi (Estate) ya SUA, kwa kushirikiana na uongozi wa Mtaa wa Mazimbu.

Uchimbaji na upanuzi wa Mto Ngerengere unalenga kuwezesha maji kupita kwa urahisi katika mkondo wake na kupunguza uwezekano wa mafuriko katika maeneo ya Kampasi ya Solomon Mahlangu. Hatua hiyo pia inalenga kulinda makazi, miundombinu na maeneo mengine muhimu yanayozunguka kampasi.

SUA inaendelea kuchukua hatua za tahadhari na kushirikiana na wadau wa eneo hilo katika kulinda mazingira na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa. Jitihada hizo ni sehemu ya maandalizi ya mapema ya kulinda usalama wa jamii, miundombinu na mazingira ya kampasi.








Post a Comment

0 Comments