Na: Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Masauni amesema Kituo cha
Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC)
nchini kilichopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kitakuwa ni miongoni mwa Taasisi muhimu katika
kusaidia Taifa kutokana na miradi mbalimbali
ambayo mataifa ya nje yanakuja kuwekeza
kupitia biashara ya Kaboni, ili biashara hiyo iweze kusaidia katika kukuza
kipato cha wananchi lakini pia kuchangia uchumi wa nchi kwa ujumla.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo Februari 10, 2025 wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kituo hicho kilichopo mkoani Morogoro.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya
Kilosa Shaka Hamdu Shaka ambaye alimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika ziara hiyo
amesema mkoa huo umejipanga kutumia vyema fursa hiyo ili kutekeleza na
kutafsiri kwa vitendo maelekezo na maono ya Rais Samia ya kuhakikisha biashara ya Kaboni inakuwa vyanzo vingine vya
kuinua kipato cha wananchi na kuchangia katika maendeleo nchini.
"Ni fursa muhimu sana kwetu uwepo wa kituo hiki mkoani kwetu ni hatua muhimu sana, kwani vianzio vyote vinavyopelekea biashara hii kufanyika tunavyo kupitia misitu, mifugo na mito tutahakikisha fursa hii inatumika vyema na tija iweze kuonekana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kupitia rasilimali tulizonazo" , alisema Shaka.
0 Comments