UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE (SUA)
INSTITUTE OF CONTINUING EDUCATION
P.B.OX 3044 CHUO KIKUU, MOROGORO, TANZANIA
TEL: +255-2603511/4 General; +255-23-2604549 (Direct),
E-mail: ice@sua.ac.tz,webpage/http://www/sua.ac.tz
MAFUNZO KOZI YA MUDA MFUPI: UFUGAJI BORA WA SAMAKI
TAREHE YA MAFUNZO 25 – 28 Novemba 2024. MAHALI: SUA Kampasi ya Edward Moringe,Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), Ukumbi wa Giraffe
LENGO KUU LA MAFUNZO: Kujengea uwezo mkulima, mfugaji au mtu yeyote kuweza kufuga samaki bora na wengi kwa ajili ya lishe
na kujiongezea kipato baada ya kuuza.
MADA ZITAKAZOFUNDISHWA: (i) uchimbaji sahihi wa mabwawa ya samaki (ii) namna bora ya usafirishaji wa vifaranga vya samaki (iii) namna bora ya kupandikiza vifaranga kwenye bwawa; (iv) utunzaji bora wa bwawa na vifaranga vya samaki (v) namna bora ya kutunza kumbukumbu (vi) utengenezaji wa chakula cha samaki (vii) mifumo mbalimbali ya uzalishaji wa samaki; (viii) urutubishaji na uvunaji wa samaki; (ix) masoko na mtaji
WALENGWA WA MAFUNZO:
Mafunzo haya yanawalenga wadau wafuatao: wakulima,wafugaji, wajasiriamali, maafisa ugani,watafiti, vikundi vya ufugaji vya vijana, wanawake, wazee na watu wengine. Pia sekta binafsi na mashirika ya serikali wote wanakaribishwa kuleta wadau wao kwa pamoja kupata mafunzo haya.
JINSI YA KUOMBA:
Jaza fomu inayopatikana kwenye tovuti /http://www. ice.sua.ac.tz au tuma kwa barua pepe ice@sua.ac.tz au piga simu kwa: Dkt. Emmanuel Malisa 0754 877 404. Miss. Sauda 0768 503 292 au Mr. James Philip 0713 627 450.
GHARAMA ZA MAFUNZO: TZS 200,000/= kwa mtu mmoja. Pia washiriki watajitegemea kwa malazi na chakula.
JINSI YA KULIPIA: Muombaji atapatiwa ankra ya malipo (control number) baada ya kuwasiliana na wahusika hapo juu.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 23 NOVEMBA 2024
Baada ya mafunzo mshiriki atapata cheti kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo na vitini rejea vya maada husika.
0 Comments