Na:Ayuob Mwigune
Vijana wapatao 600,000 kutoka mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Ruvuma, na Kigoma wanatarajiwa kufaidika na mradi wa “Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture” (YEFFA), unaotekelezwa na Ushirika wa Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO) kwa ushirikiano na AGRA Tanzania. Mradi ambao unaofadhiliwa na MasterCard Foundation kwa kiasi cha dola za Kimarekani 399,960.
Akizungumza na SUAMEDIA Bi.Irene Faustine ambaye ni mratibu wa mradi huo kutoka SUGECO, amesema mradi huo ni utakuwa kipindi cha miezi 36 kuanzia Septemba 2024 hadi Agosti 2027 ambapo,YEFFA inatarajia kuzalisha fursa za ajira 78,473 kwa vijana katika sekta ya kilimo biashara na kuwajengea ujuzi muhimu wa kuboresha maisha yao.
Kwa upande mwingine, Mhandisi Richard Semangwe, akimuwakilisha Katibu Tawala Msaidizi wa Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, amesema mkoa umepokea mradi huo kwa furaha. Ameipopongeza SUGECO kwa juhudi zao na kusema kwamba mradi huu utawasaidia vijana katika halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro.
0 Comments