Na, Josephine Mallango
Wafugaji na wakulima wametakiwa kuzingatia Matumizi ya wataalum endapo wanataka uzalishaji wa tija.
Hayo yamesemwa na Dr. Hamis Tindwa Mkurugenzi , Kurugenzi ya Shahada za Awali Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati wa kongamano la utoaji wa zawadi kwa wanafunzi watano Bora waliofanya vizuri kutoka katika ndaki ya tiba ya wanyama (VETI)
"Kwa lugha ya mtaaani mnasema kutoboa , kwa namna ya pekee kwa Sasa kufuga au kulima hauwezi kutoboa bila kutumia ushauri wa kitaalamu , mazoea hayatakiwi endapo unataka kuzalisha kwa mafanikio na tija " wataalam wapo wengi nchini kwa Sasa, Sua inazalisha wataalam kila mwaka na wako katika maneno yote nchini" Dr. Tindwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Ndaki ya TIba ya Wanyama (VETI) Prof. Esron Karimribo amesema kongamano hilo la zawadi limefanyika kwa mara ya kwanza kwa Sua kushirikiana na Ashish life science kwa wanafunzi watano waliofanya vizuri lengo ikiwa ni kuwapa chachu na kuwaandaaa wanafunzi watakaokwenda sokoni wanaomaliza Ili wakafanye vizuri zaidi na motisha kwa wanaendelea kusoma wanaobaki chuoni.
Ameongeza kuwa Chuo kimekuwa kikiingia mashirikiano na sekta mbalimbali lengo ikiwa ni kwa pamoja kupata fulsa na kukuza maendeleo ya nchi ambapo kupitia mashirikiano na Ashish life science Kuna fulsa ya kujiendekeza kimasomo kwa wanafunzi wa ndaki ya tiba ya wanyama nje ya nchi.
Mwanafunzi mhitimu wa Shahada ya Udaktari wa Mifugo katika Ndaki ya Tiba na Wanyama VETI aliyeshika nafasi ya kwanza kwa wote David Joshua Junior amesema ilikuwa ni ndoto yake kusoma SUA na sasa yuko tayari kuwatumikia Wafugaji Ili kusaidia sekta ya kilimo kuendelea kuimalika.
"SUA ni sehemu sahihi kwa vijana wanafunzi wanaohitaji mafanikio ya kielimu kwa kuwa Chuo cha SUA wakati tunafundishwa darasani pia tunaaandaliwa tutakapomaliza kukabiliana na soko la ajira kwa vitendo kwa kujiajiri wenyewe au katika ushindani wa ajira " David Junior .
Nae mwanafunzi wa kike aliyeibuka kidedea Zaituni Bakari Yasini mwanafunzi wa Diploma amewaasa wanafunzi wengine wa kike kutoongopa masomo ya Sayansi kwa kuwa kila kitu kinawezeka kwa yoyote kupata panapokuwa na juhudi huku akishukuru Elimu aliyoipata Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) imemjengea pia kuniamini.
0 Comments