Na: Josephine Mallango
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea na juhudi
za kuweka mazingira jumuishi na salama kwa wanafunzi wenye mahitaji
Maalumu ili kuhakikisha wanafikia malengo yao .
.jpg)
Akizungumza na SUA Media Mratibu wa Kitengo cha Elimu
Jumuishi na Mahitaji maalum chini ya mradi wa HEET Dkt. Thabita Lupeja amesema
wanaendelea kutoa Elimu kwa wanafunzi wote wenye mahitaji na wasio na mahitaji
maalum ili kila mtu ajisikie kuwa na haki sawa.
Dkt. Lupeja amesema katika zoezi la upimaji macho na masikio,
changamoto kubwa iko katika masikio ambapo imekuwa ni vigumu watu kupokea
matokeo ya kuwa na changamoto ya usikivu kutokana na hali hiyo kuwakuta wakiwa
watu wazima .
"Zoezi la upimaji linaloendelea limeanzia Mazimbu na
litafika mpaka Kampasi ya Edward Moringe, limeambatana na watalaam wakiwemo
kutoka UDSM ambao Wana vifaa maalum vya kupimia changamoto kubwa ni
watu kukubali hasa kwenye tatizo la kusikia kwa kuwa linawakuta wakiwa
wakubwa lakini zoezi hilo limeambatana pia na watalaamu wa kutoa
ushauri kwa namna mtu anavyokutwa na kiwango cha tatizo
wanamshauri namna ya kuendelea kulinda usikivu na kuendelea na
maisha ya kawaida" , amesema Dkt. Lupeja.
Mratibu huyo wa Kitengo cha Elimu Jumuishi na mahitaji
amesema wametoa mafunzo kwa wanafunzi wasio na changamoto ili waweze kuwa na
utu wa kuwasaidia wenzao wenye changamoto.
"Kuna mwanafunzi mmoja mwenye mahitaji maalumu
amelalamika kujibiwa vibaya na mwenzake alipomuomba msaada wakiwa kwenye foleni
wakati anaona wazi mwenzie ana changamoto, hiyo ni miongoni mwa baadhi ya
matukio yaliyochochea mradi kuona hata wanafunzi wasio na changamoto wanatakiwa
kupata Elimu ya kuwa msaada kwa wenzao kwa kuwa changamoto au ulemavu
siyo kipimo cha mtu kutokuwa na uwezo", amesema Mratibu huyo.
Nao wanafunzi waliopima na kuzungumza na SUA Media wamekishukuru
Chuo Kikuu cha Sokione cha Kilimo kwa kufanya zoezi la upimaji bure kwa madai
kuwa vipimo hivyo vina gharama kubwa na wao wasingeweza kumudu gharama hizo.
"Vipimo hivi ni bei mbaya hasa usikivu masikio hii fursa
Chuo wametupatia nawaomba wanachuo wenzangu wajitokeze kupima kujua
ugonjwa mapema kuna faida unatibu kuliko kuchelewa inatumia muda mrefu
kidogo kutatua changamoto", amesema
Onike Joseph mwanafunzi wa SUA.
Zoezi la upimaji wa baki ya uoni na usikivu linaendelea Kampasi
ya Edward Moringe kwa siku 2 ambazo ni Mei 9 na Mei 10, 2024 na linafanyika bure kwa wanafunzi wote likiwa na lengo la
kuwabaini wanafunzi wenye changamoto ili kuwasaidia kufikia malengo kwa
kuwekewa mazingira salama na jumuishi
ili waendelee kusoma pasipo kuathiri masomo yao na kuwa na haki
sawa kwa wanafunzi wote.
0 Comments