Na: Tatyana Celestine, Winfrida Nicolaus
Wanataaluma
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kuwatambua wanafunzi wenye
mahitaji maalumu katika kutengeneza usawa kwa kutoa elimu stahiki kwani Serikali
ya Tanzania kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) imewezesha
Vyuo vikuu kuhakikisha vinamjali na kumpatia elimu mwanafunzi mwenye mahitaji
maalum kama wanafunzi wengine.
Katika
kuhakikisha hilo linatekelezeka kikamilifu kwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu
Hassan Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea kutoa elimu katika
kuwajengea uwezo wanataaluma ili kuwatambua na kuwahudumia wanafunzi wenye
mahitaji maalum kulingana na mahitaji yao pamoja na kuwawezesha kutimiza
malengo.
Amebainisha
hayo Mratibu wa Kitengo cha Elimu Jumuishi na Mahitaji Maalum chini ya Mradi wa
Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) ambaye pia ni Mhadhiri
Mwandamizi na Mkuu wa Idala ya Mitaala na Ufundishaji Dkt. Thabita Lupeja na
kusema kuwa wanataaluma wanatakiwa kufahamu kwamba wao ni watatuzi wa
changamoto ambazo wanafunzi wanakumbana nazo na ni muhimu kupata suluhisho la
changamoto hizo.
Kwa upande wake Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Elimu SUA Dkt. Jamal Jumanne amesema jamii jumuishi kama SUA kuna watu wenye mahitaji maalum hivyo elimu iliyoandaliwa kwa wanataaluma itakuwa ni chachu katika kusaidia usawa unapatikana kwa kila mwanafunzi bila kujali jinsi, umri, pia uwezo hivyo kitu pekee kinachohitajika ni huduma bora yenye uwezo wa kumfika kwa wakati na urahisi.
Naye Mkuu
wa Idara ya Misingi ya Elimu na Ufundishaji ambaye pia ni Mhadhiri wa SUA Dkt.
Imelda Gelvas amesema SUA kuna wanafunzi wenye mahitaji maalum hivyo mafunzo
hayo yamewawezesha kujifunza ni jinsi gani wataweza kuwajumuisha wanafunzi wote
katika suala la kujifunza, kufahamu majina stahiki kwa wale wote wenye mahitaji
maalum pamoja na nyenzo sahihi katika mazingira ya ufundishaji ili waweze
kufikia malengo.
“Mafunzo
haya yamekuwa na mchango mkubwa sana katika kutuongezea uwezo juu ya namna ya
kutoa huduma kwa wanafunzi wetu wenye mahitaji Maalum hivyo niiombe Menejimenti
iwasaidie pia wanafunzi lakini pia wafanyakazi wengine kupata elimu kama hii
ili kurahisisha utendaji wa kazi katika kufikia lengo la kila mmoja mmoja
lakini pia Taasisi”, amesema Dkt. Imelda Gelvas.
0 Comments