SUAMEDIA

SUA yapokea magari mawili na vifaa vya kuendeleza kazi ya tafiti za misitu

 Na George Joseph

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepokea magari mawili aina ya Toyota Hilux pick up na vifaa vya kuendeleza kazi ya tafiti za misitu zinazofanywa na wataalam chuoni hapo kutoka  Shirika la Forest Development Trust, kupitia Mradi wa Tree Improvement.

                             

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Amandus Muhairwa, Rasi wa Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii Prof. Agnes Sirima amesema kuwa magari hayo ni matokeo ya ushirikiano waliyoingia mwishoni mwa mwaka 2023 na vimepokelewa maalum kwa ajili ya Idara ya Misitu.

Aidha ProfSirima amelishukuru Shirika la Forest Development Trust, kwa kuona SUA ni Chuo chenye watafiti wazuri wa misitu na kuwachagua kwa kuwapatia magari na vifaa hivyo kwani ni muhimu katika kuendeleza shughuli za tafiti na kusaidia kufanyika kikamilifu hivyo wadau wengine wajitokeze kuwezesha shughuli hizo ili SUA izidi kuwa bora katika upande huo.

                          

Pamoja na mambo mengine mwakilishi kutoka Forest Development Trust Bi Olive Luena amesema SUA ni Chuo bora katika utafiti hivyo magari na vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya maendeleo ya wanafunzi wanaofanya tafiti zao za misitu na watanzania kwa ujumla.


 







Post a Comment

0 Comments