SUAMEDIA

SUA kuingia makubaliano na Chuo cha China ZZULI

Na: Winfrida Nicolaus

Chuo Kikuu cha Zhengzhou cha nchini China (Zhengzhou University of Light Industry (ZZULI) kimetembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa lengo la kuona maeneo ambayo wanaweza kufanya mashirikiano ikiwemo kubadilishana uzoefu kwa kubadilishana wakufunzi na wanafunzi lakini pia kufanyaji wa tafiti mbalimbali.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa Manejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Febluari 23, 2024 Makamu Mkurugenzi wa Taaluma Bw. Wang Jiwei ameipongeza SUA kwa kuleta mafanikio makubwa nchini Tanzania kutokana na mchango wake kupitia tafiti mbalimbali wanazozifanya hivyo wangetamani kuwakaribisha kwenda kuwatembelea na kujionea vitu ambavyo wao wanavifanya na kuweza kushirikiana kwa pamoja.

 Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA, Prof. Raphael Chibunda amekishukuru chuo hicho kwa kutoa mwaliko kwao kwa ajili ya kwenda kujifunza kutoka kwao vilevile wanamatarajio ya kuona wanafunzi wao pamoja na wafanyakazi kutoka SUA wanaenda kujifunza mafunzo ya muda mfupi pia ikiwezekana wafanyakazi kutoka ZZULI Kwenda SUA kutoa mafunzo. 

Vilevile amekishukuru Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM) kwa kuonesha ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha ugeni huo unawafikia baada ya kuona kuwa kuna maeneo ambayo wanaweza wakashirikiana baina ya Chuo Kikuu cha ZZULI na  SUA.


 






Post a Comment

0 Comments