SUAMEDIA

SUA, JKUAT kuendelea kubadilishana uzoefu na maarifa

 Na, Godfrey Msinjili


Chuo Kikuu cha Sokoine cha  Kilimo (SUA) na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia (JKUAT) kuendeleza mashirikiano kwa lengo la kubadilishana wanataaluma, wanafunzi, kushirikiana katika tafiti za kilimo na uhandisi ili kubadilishana uzoefu na maarifa.

 


Akizungumza na SUAMEDIA, Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi Shirikishi, SUA Prof. Esron Karimuribo, amesema kuwa vyuo hivyo vimedumisha mashirikiano hayo  takribani miaka kumi  kwa sasa wapo katika mchakato wa kufanya mashirikiano hayo kuwa rasmi na kuongeza miaka mitano kuendelea kujikita katika kutengeneza mitaala, kufundisha kwa pamoja katika sekta mbalimbali na tafiti na bunifu. 


Pamoja na mambo mengine Prof. Karimuribo  ameongeza kuwa makubaliano hayo yaahusu pia matumizi ya teknolojia ya kisasa ya akili bandia (Artificial Intelligence) katika fani za uhandisi na mabadiliko ya tabia nchi na kujikita katika sayansi ya majini (Marine Sciences). 

 

Kwa upande wao Naibu Makamu Mkuu  Taaluma kutoka JKUAT Professa Robert Kinyua, na Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA) Mai Toda Nakano, wamesema kuwa ushirikiano huo utakuwa  mahususi kwa ajiri ya kuunda mtandao wa Elimu ya juu na kuwezesha wanafunzi kujifunza kutoka sehemu mbalimbali kwa pamoja.



                                  





Post a Comment

0 Comments