SUAMEDIA

SUA yaadhimisha Siku ya Udongo duniani kwa kutoa Elimu kwa jamii


Na, Winfrida Nicolaus

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia imeadhimisha Siku ya Udongo Duniani ambayo huadhimishwa Disemba 5, kila mwaka na kuelimisha makundi mbalimbali ya watu kutoka kwenye jamii inayowazunguka  kuhusiana na umuhimu wa kuhifadhi udongo ili kuhakikisha unaendelea kuleta tija kwa maisha ya mamilioni ya watu duniani wanaotegemea chakula  kutoka kwenye kilimo.

Amesema hayo Dkt. Mawazo Shitindi Mhadhiri toka Ndaki ya Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati akizungumza na SUAMEDIA ambapo amesema maudhui ya mwaka huu 2023 ni “Udongo na maji ni chanzo cha uhai” hivyo uwepo wa dunia unategemea uhusiano uliopo baina ya rasilimali muhimu ya udongo na maji kwani zaidi ya asilimia 95 ya chakula duniani inategemea uwepo wa rasilimali hizo mbili.

Amesema Udongo usipotunzwa vizuri uwezo wake wa kufanya kazi ikiwemo kurutubisha mimea kwaajili ya maisha ya viumbe hai ikiwemo binadamu unapungua  na si tu kupungua kuna wakati utashindwa kufanya kazi au kufa kabisa hivyo ukifa ina maana maisha ya binadamu pomoja na viumbe hai wengine yanakufa pia kwakuwa yanategemea sana Udongo.

“Mimea inamea kwenye Udongo kwa kupata virutubisho na madini mbalimbali kwenye udongo hivyo sisi binadamu tunakula mazao yatokanayo na hiyo Mimea yenye virutubisho na madini kutoka kwenye huo udongo ukweli ni kwamba sisi hatuna uwezo wa kutengeneza Chakula moja kwa moja bali tunategenea Mimea ambayo inategemea Udongo ili iweze kuishi”, alisema Dkt. Shitindi

Aidha Dkt. Shitindi amesema Wanasasayansi pamoja na watumiaji wengine wa udongo wameona ni muhimu kuwepo kwa Siku  ya Udongo  ili kukumbushana na kutafakari kuwa Udongo unafanya nini kwa maisha ya binadamu na wafanye nini kwaajili ya udongo huo ili kuufanya uwe endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Tukiwa kama Taasisi ya kutoa elimu SUA ni kuwa tubawaandaa Wataalam ambao wataenda kufanya kazi mbalimbali wakitoka chuoni hapo wakiwemo watakaoenda kuwafundisha Wakulima moja kwa moja vilevile watakaoenda kufanya kazi kwenye mashirika mbalimbali hivyo lengo letu ni kuweka maarifa kwa hawa vijana ili wanapoondoka waende kuelimisha umma juu ya kazi kubwa ya Udongo kwa maisha ya mwanadamu vilevile wahakikishe wanakitu cha kufanya ili kuhakikisha Udongo unakuwa endelevu.

Kwa upande wake Avida Yanda Mwanafunzi wa mwaka wa pili toka Ndaki ya Kilimo anayechukua Shahada ya Sayansi ya Udongo na Mimea amesema siku hiyo imekuwa yamuhimu kwao wakiwa kama wataalamu wa Udongo ambao wataenda kuelimisha jamii hasa ya wakulima juu ya kulima kwa Afya kwa kizingatia utunzaji wa ubora wa udongo kwa ajili ya kuzalisha kwa wingi lakini pia kwa tija huku ubora wa udongo ukibaki palepale kwa matumizi ya sasa na baadae.

Naye Wilbert Rubanzibwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu Kozi ya Sayansi ya Udongo na Mimea SUA amesema Udongo ni kitu ambacho kinaendelea kupungua kila siku kutokana na ongezeko la watu na shughuli nyingine za kiuchumi hivyo kutokana na ongezeko hilo la watu udongo unaendelea kuharibiwa kwa namna mbalimbali kwasababu ya shughuli za kibinadamu ndio maana ipo siku hiyo muhimu ya udongo yenye lengo la kuikumbusha jamii kuwa Udongo ni maisha ukiharibiwa na maisha yanaharibika.

Amesema jamii inatakiwa kuelimishwa kuhusiana na vitu ambavyo vinaleta uharibifu wa udongo ikiwemo shughuli za kilimo ambazo zinaweza zikasababisha mmomonyoka wa udongo endapo kilimo hicho akikufanywa kitaalam ukataji wa miti vilevile matumizi ya mbolea kiholela hivyo nitoe wito kwa jamii kuendelea kupata elimu pindi inapotolewa hasa kwa siku maalum kama hiyo.









Post a Comment

0 Comments