Na: Calvin Edward Gwabara - Nairobi
Woga usiojulikana unsababisha
Viwavijeshi vamizi kushambulia zaidi ya tani milioni 20 za Mahindi ya wkakulima
ambayo yengeweza kulisha zaidi ya watu milioni 100.
Meneja wa Mradi wa Mahindi wa TELA Dkt. Sylvester Oikeh wakati akiwasilisha mada. |
Hayo yamebainishwa na Meneja wa
mradi wa Mahindi wa TELA Dr. Sylvester Oikeh wakati akiwasilisha mada kuhusu
uwezeshwaji wa uhimilivu wa changamoto za kilimo kupitia Sayansi Teknolojia na
Ubunifu wakati kwenye Mkutano wa Teknolojia za Kilimo Barani Afrika unaoendelea
Jijini Nairobo Nchini Kenya.
“ Pamoja na Mamlaka mbalimbali
duniani za uthibiti ubora kuthibitisha kuwa mazao yatokanayo na Tenkolojia ya
Uhandisi jeni ( GE) kuwa ni salama kwa binadamu na mazingira lakini bado
teknolojia hiyo inazuiliwa na baadhi ya watu kwa kuwatisha wananchi hasa
wakulima kuhusu usalama wake” Alieleza Dkt.
Sylvester.
Aliongeza “Kuna nchi hadi sasa hazitumii
teknolojia hiyo ingawa tafiti zimekamilika kwa sababu moja tuu ya kutokuwa na
sheria ambayo inaruhusu au kuwa rafiki kwenye hatua ya ubiasharishaji wa mazao
ya bioteknolojia yaani GMO”.
Amesema kuwa zao la mahindi ndilo
linaloshambuliwa zaidi na kiwavijeshi vamizi kutoka amerika na ni zao ambalo
linategemewa kwa chakula na na zaidi ya watu milioni 300 barani afrika hivyo
jitihada za makusudi zinahitajika katika kutumia teknolojia kuwakabili wadudu
hawa ambao wanasabaisha njaa na umasikini kwa wakulima.
PICHA WASHIRIKI WAKIFUATILIA WASILIHO.
0 Comments