SUAMEDIA

Vijana watakiwa kuwa mhimili wa Kilimo Afrika.

 Na: Calvin Gwabara - Nairobi

Ongezeko kubwa la ukuaji wa vijana ambao ni nguvukazi katika kufufua uchumi wa Bara la Afrika hakujatumika vilivyo hali inayotokana na vijana kutoshirikishwa ipasavyo katika shughuli za kilimo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa AATF Dkt. Canisius Kanangi akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo Jijini Nairobi Nnchini Kenya.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Teknolojia za Kilimo Africa (AATF) Dkt. Canisius Kanangi wakati akitoa utambulisho kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Teknolojia za Kilimo Africa (ACAT) jijini Nairobi.

“Hali hii inapelekea Bara la Afrika likihangaika kulisha watu wake na hivyo kuwa muagizaji mkubwa wa chakula kwa ajili ya watu ijapokuwa ina ardhi kubwa yenye rutuba Duniani”alisema Dkt.Kanangi.

Aidha amesema kuwa AATF inaaamini katika matumizi ya Sayansi, teknolojia na ubunifu hasa kupitia shuhuda kutoka kwenye nchi zaidi ya 24 za Afrika ambazo wamekuwa wakifanyakazi na Serikali na Taasisi za utafiti za nchi hizo katika kuwaelekeza wakulima kuboresha kilimo chao.

Akizungumza kwenye mjadala wa kwanza iliyoangalia uwezeshwaji wa wakulima kuhimili changamoto za kilimo kwa kutumia Sayansi Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt.Amos Nungu amesema Tanzania ikombele katika kusaidia idadi kubwa ya vijana nchini kushiriki kwenye kilimo cha kisasa na kujiletea maendeleo.

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt.Amos Nungu akieleza namna Tanzania inavyotumia STI katika kupunguza changamoto za wakulima.

“Tanzania inatambua nguvu ya vijana ndio maana imeanzisha programya (Building a Better Tomorrow) kwa lengo kuwapa mazingira rafiki ya kufanya kilimo kwa kuwapatia miundombinu na mitaji ili waweze kushiriki katika kujiletea  maendeleona kujenga taifa” alifafanua Dkt.Nungu.

Ameongeza kuwa Serikali kupitia COSTECH imekuwa ikitoa fedha kuwezesha watafiti na wabunifu kufanyiakazi bunifu mbalimbali zenye tija ilikuhakikisha Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unatumiwa na kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii na kuwapatia kipato lakini pia tayari kuna makampuni machanga (startups) yanayotoa huduma katika masuala ya kilimo.

Mkurugenzi huyo amewaambia wadau wa  mkutano huo mkubwa wateknolojia za Kilimo Afrika kuwa COSTECH kama mshauri mkuu wa Serikali kwenye masuala hayo  wamewezesha kufanyika kwa tafiti nyingi zenye tija kwa taifa ikiwemo Utafiti wa Mradi wa Mahindi yanayotumia maji kwa ufanisi Afrika (WEMA) ambao umesaidia kupatika na kwa ina 11 za mbegu ambazo zinatumiwa na wakulima nchini Tanzania.

Kwenye mkutano huo mkubwa wa Teknolojia za Kilimo Barani Afrika unaofanyika Nchni Kenya na  kukutanisha wadau kutoka  Afrika na duniani kote, Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ambaye ameambatana na Mkurugenzi  Mkuu wa COSTECH pamoja na  Maafisa kutoka Wizara ya Kilimo na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Rais wa Zamani wa Nigeria Mhe. Dkt. Dr. Goodluck Jonathan akifuatilia mawasilisho na mijadala kwenye Mkutano huo.









Post a Comment

0 Comments