SUAMEDIA

Wakulima Afrika waomba kushirikiswa kwenye maamuzi yanayowahusu.

 Na: Calvin Edward Gwabara.

Wakulima Barani Afrika wameomba Bioteknolojia ipewe nafasi na kujumuishwa kwenye menyu ya zana za kilimo zilizopo ili waweze kuchagua kulingana na mahitaji badala ya kuwekewa vipingamizi huku ikinufaisha wakulima kwenye nchi zingine.

Mkulima wa kiongozi wa Pamba ya Bt kutoka Kenya Bwana  Daniel Magondu (Wa pili kutoka kushoto aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kwenye mjadala huo wa wakulima wa Afrika, Wengine ni wakulima wenzio kutoka nchi mbalimbali.

Ombi hilo limetolewa na wakulima kutoka mataifa mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia za Kilimo Barani Afrika Jijini Nairobi wakati wa mjadala wa wakulima uliohusu umuhimu wa kuwapa wakulima nafasi sahihi katika masuala yanayohusu kilimo.

Akizungumzia umuhimu huo Mkulima wa kiongozi wa Pamba ya Bt kutoka Kenya Bw. Daniel Magondu amesema wanapata changamoto kubwa ya kufikia teknolojia zenye za kisasa na pembejeo zingine hali ambayo inawafanya washindwe kuzalisha kwa tija.

“Huwa najiuliza sana kama kuna teknolojia ambayo inakinzana na wadudu, Mabadiliko ya tabia nchi na magonjwa kwanini nashea jasho langu na visumbufu hivyo vya mazao? Lakini jibu likawa ni zuio la Serikali kwa wakulima kutumia mbegu hizo za zinazotokana na uhandisi jeni” Alieleza Bwana Fatch.

Aidha amesema kuwa wakati wakulima wa nchi zingine duniani wanafaidi matunda ya Sayansi na teknolojia kwenye matumizi ya mbegu hizo wakulima wengine wanaendelea kuteseka na changamoto hizo za kilimo na kuwafanya washindwe kupiga hatua na kuona kilimo ni mateso.


Muongozaji wa Mjadala huo akizungumza na wakulima hao wakati wa majadiliano.


  Rais wa Zamani wa Nigeria Mhe. Dkt. Dr. Goodluck Jonathan akifuatilia majadiliano hayo ya wakulima kwenye Mkutano huo.








Post a Comment

0 Comments