Na Gerald
Lwomile - Arusha
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kuthibiti Uadilifu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Christpher
Mahonge amesema ni muhimu wafanyakazi wawe na roho ya kusikiliza ili kujifunza
zaidi na kuwa na maelewa katika maeneo ya kazi ili kuleta tija.
Prof. Mahonge amesema hayo leo Septemba 29, 2023 wakati akizungumza na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Kampasi ya Olmotonyi mkoani Arusha.
Amesema ni muhimu watu kujua namna njema na sahihi ya kuishi pamoja na kuchukuliana ili kuleta tija katika kazi kwani ili taasisi iweze kutimiza malengo yake ni lazima kuwa na hali ya kutegemeana miongoni mwa watumishi.
Meneja wa Kampasi ya Olmotonyi Bw. Said Kiparu akizungumza kabla ya kuanza mafunzo |
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu SUA Prof. Mahonge akitoa mafunzo ya Uadilifu |
0 Comments