SUAMEDIA

Shule ya Sekondari Kilakala yatembelea SUA, yasifu kozi zinazotolewa na Chuo hicho

 Na Winfrida Nicolaus

Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala iliyopo Mjini Morogoro wametembelea Banda la SUA katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki na kusifu kazi nzuri zinazofanywa na Chuo hicho kwa kutoa Kozi mbalimbali na za kuvutia tofauti na  Kilimo ambayo ni kozi mama na hivyo kuwapa shauku ya kujiunga na SUA.

                      

Amebainisha hayo Asia Senya mwanafunzi wa Kidato cha Sita mchepuo wa CBG akiwakilisha wenzake kuzungumza na SUAMEDIA kile walichojifunza wakati walipotembelea Banda la SUA kwenye Maonesho hayo yanayofanyika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mkoani Morogoro.

Amesema wakiwa kama wanafunzi wanaotarajia kwendaVyuo vikuu wamejifunza kuhusu kozi nyingi zinazotolewa SUA ambapo si Kilimo pekee au Udaktari wa Mifugo ni mambo mengi na ya kuvutia hivyo wanashauku ya kuelezea jamii hasa wanafunzi wenzao waijue vizuri SUA ilivyopana na ndio Chuo pekee mpaka wakati huu kinachowafanya vijana wapate ajira pamoja na kujiajiri wenyewe moja kwa moja pindi tu wanapomaliza masomo yao.

Kwa kweli kilichotuvutia zaidi SUA sio Elimu tu SUA ni ajira kwa kuwa ina mambo mengi tunaweza kusema Chuo hiki ni Utalii wa kutosha yaani Wild life inafanyika ndani ya SUA, kuna sabuni tumeona, vitu vya asili vinafanyika pale vimetuvutia kwa kweli tulijua SUA ni kitu kimoja ambacho ni Kilimo lakini sio kweli mambo ni mengi na ni mazuri, amesema mwanafunzi huyo.

Asia ametoa wito kwa wanafunzi wenzao kutoka Shule zingine kutembelea Banda la SUA kwenye Maonesho ya 88 ili wapate kujua Elimu na jinsi dunia inavyoenda na cha muhimu zaidi wapende kufuatilia mambo ili kuweza kufahamu nini kinaendelea katika jamii na kuujua vizuri ulimwengu wa Sayansi.

Vile vile amewaomba Wakulima nchini kutembelea SUA kwa kuwa ni sehemu ambayo wanaweza wakajifunza vitu vingi kuhusu Kilimo na jinsi gani wanaweza kuzalisha kwa Tija na kuhifadhi salama Mazao yao kwa kutumia njia rahisi zaidi zisizo na gharama kubwa.









Post a Comment

0 Comments