Na: Winfrida Nicolaus
Jamii
imetakiwa kutumia zaidi dawa za asili zinazotokana na miti dawa ambazo
zimethibitishwa na Shirika la Viwango Nchini (TBS) kwa sababu dawa hizo za
asili hutumika kama chakula tofauti na dawa nyingine na hazina madhara mwilini.
Wito huo umetolewa Agosti 7, 2023 na Fundi Maabara kutoka Idara ya Kemia na Fizikia katika Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bi. Aneth Coster wakati akizungumza na SUAMEDIA katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kwenye Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayofanyika mkoani Morogoro kuhusiana na bidhaa mbalimbali za dawa za asili zinazotengenezwa na Idara hiyo.
Bi.
Aneth amezitaja dawa zilizopo katika maonesho hayo kuwa ni Synadol ambayo hutumika
kwaajili ya kutibu Mfumo mzima wa upumuaji yaani inatibu kikohozi, mafua
makali, pumu pamoja na mafindofindo ambayo imetengenezwa kwa kutumia mti dawa
baada ya kufanyiwa tafiti za kutosha na kubaini mti huo una uwezo wa kutibu
magonjwa hayo.
“Pia
tuna dawa nyingine inayotibu ngozi ambayo ipo katika mfumo wa sabuni na
imetengenezwa kwa kutumia mti dawa unaoitwa Mvunja kongwa ambao kitaalamu
unalikana kwa jina la Synadenium na majani yake nayo yamefanyiwa tafiti na
kuona yanatibu kwa hiyo sabuni hizi zimetengenezwa kwa kutumia majani na mizizi
na zinatibu ngozi kama imeathirika na fangasi”, amesema Bi. Aneth.
Dawa
nyingine ambazo zimetengenezwa na Idara hiyo ya Kemia na Fizikia ni dawa ya
kusafisha na kungarishia sinki la chooni hasa likiwa na uchafu korofi, pamoja
na vitasa mikono (sanitizer).
“Tafiti
zinaendelea na pia tuna kitu kinaitwa indicator
(viashiria) hivi vinatumika kwenye kuweza kuchanganya tindikali mbili base na acid ili upate neutralization
yaani upate end point kwa hiyo tuna indicator ile ambayo imetengezwa kwa
miti nia yetu kubwa ni kwamba badala ya kuendelea kutumia indicator ambazo tunazinunua toka nje tufike mahala tutumie bidhaa
zetu za ndani ili kupunguza gharama”, amesema Bi. Aneth.
0 Comments