Na: Farida Mkongwe
Chuo Kikuu cha Sokoine
chaKilimo (SUA) kupitia Kitengo cha Ukuzaji wa Viumbe Maji kilichopo Idara ya
Mashamba ya Mafunzo kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Nanenane kimekuja na
Maabara inayotembea maalum kwa ajili ya utotoreshaji wa vifaranga vya samaki
aina ya sato.
Maabara inayotembea maalum kwa ajili ya utotoreshaji wa vifaranga vya samaki aina ya sato ikiwa kwenye Maonesho ya Nanenane banda la SUA |
Hayo yamebainishwa Agosti 4, 2023 na Afisa Mafunzo wa Kitengo hicho Bi. Stella Genge wakati akizungumza na SUAMEDIA katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere mjini Morogoro.
Bi.Stella amesema lengo ya
kupeleka Maabara hiyo kwenye maonesho ya Nanenane ni kutaka kukidhi kiu ya
wakulima ambao kwa muda mrefu walikuwa na hamu ya kuona namna vifaranga vya
samaki vinavyozalishwa.
“Tumeona sasa tuje na Maabara
hii ndogo portable ambayo tunaweza tukatembea
nayo ina matairi kabisa inatembea ili kuwaonesha ni namna gani tunazalisha
vifaranga vya samaki aina ya sato na uzalishaji wa vifaranga vya sato huwa
tunaanza na kuandaa wazazi, shughuli hiyo mara nyingi tukiwa kule Chuoni
inafanyika kwenye mabwawa makubwa lakini hapa pia tumebeba tunaonesha namna
gani tunaandaa wazazi”, amesema Bi. Stella.
Akielezea namna uzalishaji wa
vifaranga hao unavyofanyika Bi. Stella amesema wanawaweka wazazi kwa uwiano wa
dume moja na majike matatu baada ya wiki mbili wanawapokonya mayai mdomoni na
kuyaweka kwenye maabara hiyo inayotembea kwenye majagi ya kuangulia ndani ya
siku saba yale mayai yanakuwa yameanza kuangua na kuwa vifaranga na hivyo
kuanza kuvilea vifaranga kwa siku 28 na ndipo vinapouzwa kwa mteja.
Aidha Bi. Stella amesema mbali
na Maabara hiyo pia kwenye banda lao kuna samaki aina ya Sato na Kambale pamoja
na samaki wa Mapambo.
“Ukija kwenye banda letu
utafurahi mwenyewe tuna meza nzuri sana za kuweka sebuleni na kunakuwa na samaki
wa mapambo hii inasaidia sana kwa wale watu wenye umri mkubwa kuwaondolea
mawazo lakini pia vijana kuna wakati unakuta mtu umeghafirika ukiwa
unawaangalia tu hawa samaki wanakusaidia kuondoa msongo wa mawazo lakini pia
inapendezesha nyumba yako”, amesema Bi. Stella.
Afisa Mafunzo wa Kitengo cha Ukuzaji wa Viumbe Maji kilichopo Idara ya Mashamba ya Mafunzo SUA Bi. Stella Genge (Kushoto) akitoa maelezo kwa watu waliotembelea banda la Kitengo hicho. |
Mtaalamu wa Samaki kutoka SUA Bw. Elvin Vigga akiweka chakula cha vifaranga vya Samaki kwenye Maabara maalum ya kutotoreshea Vifaranga aina ya Sato. Picha zote na Nicholus Roman. |
0 Comments