Na: Calvin Gwabara – Morogoro.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia Nchini Tanzania Bw. Nathan Belete amepongeza Chuo kikuu cha Sokoine cha
Kilimo kwa kutumia fedha zilizotolewa na Benki hiyo na kuahidi kuendelea kutoa
ushirikiano ili kuendeleza matokeo mazuri yaliyopatikana.
Hayo ameyasema wakati akizungumza
na Uongozi na Watafiti wa Chuo hicho mara baada ya kupokea mawasilisho ya
utekelezaji wa fedha zilizotolewa na Benki hiyo katika utekeelezaji wa miradi
kwenye Taasisi ya afya moja inayoshughukikia magonjwa ambukizi kusini mwa jangwa
la sahara (SACIDS), Mradi wa HEET na Kwenye kituo cha umahiri cha mashariki na
kusini mwa Afrika cha kudhibiti panya na matumzi yake katika kunusa (ACE IRPM
& BTD).
“Kwa kutambua mchango wa elimu
kama mtaji wa binadamu ndio maana Benki ya Dunia tumeweka swala la elimu kama
kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi yetu hivyo nitumie nafasi hii kuahidi
Wizara ya Elimu pamoja na SUA kuwa tutaendelea kutoa ushirikiano katika
kuteleza miradi kama hii ambayo inaleta tija kubwa kwenye maendeleo ya wananchi
na Taifa” alisema Bwana Belete.
Bwana Belete amepongea kazi nzuri
inayofanywa na SUA katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za taifa
na kuahidi kushirikiana na Chuo hicho kwenye kusaidia ongezeko la udahili wa
Wanafunzi kutokana na takwimu kuonesha udahili nchini Tanziania upo chini
ikilinganishwa na nchi jirani.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Elimu ya Juu, Dkt Keneth Hosea akitoa salamu za Wizara ya Elimu ameiomba
Benki ya Dunia kuona uwezekano wa kuongeza fedha kwenye miradi hiyo ili kazi
nzuri iliyofanywa na miradi kwenye vituo hivyo vya umahiri iendelezwe zaidi.
“Kwakuwa kupitia mradi wa HEET
unakwenda kuongeza nguvu kwenye kampasi 15 mpya kwenye vyuo mbalimbali vya umma
nchini tunaomba Benki ya Dunia itusaidie kuongeza fedha kwenye eneo la Mafunzo
kwa wanataaluma pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwenye maabara
zetu” aliomba Dkt. Hosea.
Awali Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda amesema mchango wa miradi hiyo
miwili ya SACIDS na (ACE IRPM & BTD iliyofadhiliwa na Benki ya Dunia ni
mkubwa sio tuu kwa Tanzania bali kwa bara la Afrikakwani tafiti zake zinagusa Afrika.
“Naomba nitumie nafasi hii
kushukuru sana msaada tunaoupata kutoka Serikali yetu na Bank ya Dunia ambayo
inasaidia chuo kwenye kutekeleza majukumu yake na kupitia Mradi wa HEET
tunawekeza katika shamba letu la Miti huko Madaba ili ndani ya kipindi cha
miaka mitano tuongeze mapato yetu ya ndani ya Chuo na kupunguza utegemezi”
alisema Prof. Chibunda.
Katika mkutano huo Chuo kilipata
nafasi ya kutoa mawasilishao mbalimbali ikiwemo Historia, Kazi na mafanikio ya
Chuo toka kuanzishwa kwake iliyowasilishwa na Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Taaluma
Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala ambaye alieleza namna
Chuo kinavyotekeza majukumu yake.
Aidha, Mawasilisho mengine ni
Utekelezaji wa Taasisi ya afya moja inayoshughukikia magonjwa ambukizi kusini
mwa jangwa la Sahara (SACIDS) lililowasilishwa na Prof. Gerald Misinzo, Wasilisho
la Mradi wa HEET lililowasilishwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Utawala
na Fedha Prof. Amandus Mharwa na Mratibu wa Mradi huo Dkt. Winfred Mbungu na
Wasilisho la Kituo cha Umahiri cha
Mashariki na Kusini mwa Afrika cha Kudhibiti Panya na matumzi yake kanitika
kunusa (ACE IRPM & BTD kutoka kwa Prof. Appiah Masawe.
Baada ya mawasilisho hayo Mkurugenzi huyo Mkazi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Bw. Nathan Belete pamoja na ujumbe wake walipata nafasi ya kutembelea kuona vituo hivyo na kazi zinazofanyika na kuona namna fedha walizotoa zilivyosaidia kufanyika kwa tafiti zenye faida kubwa kwa taifa na Afrika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda akitoa salamu za SUA. |
Prof. Gerald Misizo akitoa wasilisho kuhusu utekelezaji wa Taasisi ya afya moja inayoshughukikia magonjwa ambukizi Kusini mwa Jangwa la Sahara (SACIDS) |
Prof. Appiah Masawe akiwasilisha Utekelezaji wa mradi kwenye Kituo cha Umahiri cha Mashariki na Kusini mwa Afrika cha Kudhibiti Panya na matumzi yake kanitika kunusa (ACE IRPM & BTD) |
Mratibu wa Mradi wa HEET Dkt. Winfred Mbungu akiwasilisha utekelezaji wa Mradi huo SUA. |
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Dkt Keneth Hosea akitoa salamu za Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. |
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Bw. Nathan Belete akizungumza mara baada ya kusikia mawasilisho yote ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia. |
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Utawala na Fedha Prof. Amandus Mharwa akiwasilisha sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa HEET. |
Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Taaluma Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala akitoa salamu na Historia ya Chuo. |
0 Comments